25.5 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Marufuku kutoka nje yaongezwa kwa siku 21

KAMPALA, UGANDA

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni ametangaza kuongeza muda wa marufuku ya watu kutoka nje kwa siku 21.

Hatua hiyo inachukuliwa kama njia ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.

Mpaka sasa watu 54 wamegunduliwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo na kati yao wanne wapemona. Hakuna kifo kilichoripotiwa kufikia sasa.

Machi 31, Museveni alitangaza marufuku ya watu kutokutoka nje kwa siku 14, ambazo zilikuwa zinaisha jana Aprili 14.

Jana, Museveni alisema bado wanahitaji muda zaidi wa kupambana na virusi hivyo na watu waendelee kusalia majumbani mwao.

Musveni alitoa agizo hilo muda mfupi baada ya mwanamuziki na mbunge wa Uganda, Kyangulanyi Ssentamu maarufu kama Bobi Wine, kusema kuwa ameungana na mfanyibiashara wa Marekani kuwarejesha nyumbani Waafrika wanaodaiwa kubaguliwa China.

Hii ni baada ya taarifa kuibuka kuwa mamia ya watu wenye asili ya kiafrika kufurumushwa kutoka majumbani mwao katika mji wa China wa Guangzhou kutokana na hofu kuwa virusi vya corona vinasambazwa na jamii ya kiafrika.

Bobi Wine alisema yeye na mfanyibiashara wa Neil Nelson wako tayari kuwasafirisha makwao watu hao ikiwa mataifa yao yatakuwa tayari kuwapokea.

Wawili hao pia wana mpango wa kuwasafirisha Marekani watu walio na uraia wa nchi hiyo ama wale waliopewa hadhi ya mkazi wa kudumu Marekani.

“Tunatoa wito kwa Serikali ya China kukomesha ubaguzi dhidi ya watu weusi,” walisema katika taarifa ya pamoja.

Nigeria, kupitia ubalozi wake mjini Beijing, ilisema inajiandaa kuwaondoa raia wake nchini China.

Hali ya taharuki imetanda katika mji wa Guangzhou kufuatia hofu inayozunguka maabukizi ya virusi vya corona.

Kwa mujibu wa kiongozi wa kijamii mamii ya Waafrika wameshindwa kurejea katika nyumba zao ama hoteli baada ya madai kuibuka kuwa jamii ya watu weusi inasambaza virusi hivyo hatari.

Mamlaka katika mkoa wa Guangdong ilijibu madai ya ubaguzi dhidi ya Waafrika na kuingeza kuwa China na Afrika ni marafiki wazuri, washirika na ndugu.

Ilisema “mataifa ya Afrika yana umuhimu mkubwa”… na kwamba juhudi zinafanywa kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hiyo na Afrika”.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles