22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

MARTIN KADINDA: WEMA AMEBADILIKA HADI RAHA

Na ESTHER GEORGE-DAR ES SALAAM


Wema Sepetu, Martin KadindaALIYEKUWA Meneja wa Mrembo wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Martin Kadinda, amempongeza mwanadada huyo kwa kubadilisha mfumo wa maisha yake.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Martin alisema kitendo cha Wema kufuta picha zake kwenye mitandao ya kijamii na kubadili tabia za kuweka wazi maisha yake ni hatua ya kupongezwa.

“Uamuzi alioufanya Wema ni hatua nzuri na ya kupongezwa, mimi na familia yake hatukuwa tukipendezwa nayo kwa kuwa ilikuwa ikichafua jina lake,” alieleza Martin.

Martin aliongeza kwamba Wema ambaye amebadili meneja kwa sasa, amekuwa tofauti na alivyozoeleka maana amekuwa muelewa na msikivu kwa anachoelekezwa.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles