MARS ILIKUWA NA UWEZO WA KUHIFADHI VIUMBE HAI

0
874

Na JUSTIN DAMIAN


MIAKA bilioni kadhaa iliyopita, sayari ya Mars ilikuwa ni sehemu nzuri ambayo viumbe hai wangeweza kuishi kutokana na uwapo wa maji ya kutosha pamoja na udongo wenye rutuba.

“Tumegundua mazingira ambayo yangeweza kufaa kwa maisha ya viumbe hai ikiwamo uwapo wa maji ambayo kama yangekuwapo duniani tungeweza kuyatumia kwa ajili ya kunywa na shughuli nyingine,” anasema John Grotzinger ambaye ni Profesa katika taasisi ya Teknalojia ya California nchini Marekani na ambaye pia ameshiriki katika utafiti kuhusu Mars kupitia Kituo cha Anga cha Marekani (NASA).

 Kupitia roboti aliyetumwa kufanya utafiti kwa kupasua mwamba na kuteta taarifa zake duniani, wanasayansi wanasema uwapo wa matope kati kati ya miamba ni ushahidi tosha kuwa miaka iliyopita sayari hiyo ilikuwa na maji ya kutosha

pamoja na maji, wanasayansi waligundua madini kama, sulfur, nitrogen, hydrogen, oxygen, phosphorus na carbon kwenye miamba ambayo ni muhimu kwa maisha.

Profesa Grotzinger anasema madini hayo ni kama betri na ni muhimu kwa maisha kwa kuwa ni chanzo cha nishati kwa mwili.

Ugunduzi mwingine muhimu ni pamoja na udongo wa mfinyanzi ambao mara nyingi hupatikana sehemu sehemu zenye maji

“Kitu muhimu ambacho tumeweza kujifunza ni kuwa, katika kipindi cha miaka 20 iliyopita baadhi ya viumbe wadogo wadogo wangeweza kupata nguvu kwa kula kupita miaka ambayo ilikuwa na madini muhimu kwa maisha,” anasema Grotzinger

Hata hivyo, wanasayansi wanasema takribani miaka bilioni tatu iliyopita, hali katika Sayari ya Mars ilibadilika. Mabadiliko hayo yalihusisha kupoa kwa hali ya hewa pamoja kusimama kwa ulipukaji wa volacano. Maji yaliganda au kutoweka kwa njia ya mvuke na kuifanya sayari hiyo kuwa kavu na yenye baridi.

Leo hii uso wa sayari hiyo ni baridi na mkavu huku ukiwa na mionzi inayotokea angani. Lakini wanasayansi wanaamini kuwa miaka bilioni tatu iliyopita ilikuwa ni sehemu nzuri kwa maisha kwa kuwa hali ya hewa ilikuwa ya baridi ya wastani pamoja na maji yaliyokuwa yakitiririka.

Ujumbe wa NASA ulioenda Mars haukuwa na chombo chenye uwezo wa kutambua kama kuna kiumbe aliwahi kuishi kwenye sayari hiyo lakini iliweza kutambua baadhi ya madini ambayo kimsingi ni muhimu kwa maisha.

Ninayo picha sasa ya kitu kama ziwa la maji baridi pamoja na hali ya hewa ya wastani kwa ajili ya maisha,” anasema John Grunsfeld, mmoja kati ya timu inayofanya utafiti juu ya Mars kutoka NASA.

Sayari ya Mars ni ya nne kwenye mfumo wa jua na ni ya pili kwa udogo. Jina la Mars lilitokana na mungu wa vita wa dola ya Warumi ya zamani. Sayari hii wakati mwingine huitwa Sayari Nyekundu kutokana na kuwa na muonekano wenye rangi nyekundu.

Pamoja na utafiti wa miaka mingi ya utafiti, hakuna binadamu aliyeefanikiwa kufika katika sayari hii kutoka na sababu mbalimbali ikiwamo hali ya hewa ya baridi pamoja na hewa na carbon dioxide.

Kama binadamu akifanikiwa kufika kwenye sayari hii, atajikuta akiwa na uzito mdogo kuliko uzito wake halisi kutokana na nguvu ya gravity. Endapo ana kilo 45 akifika Mars atajikuta akiwa na kilo 17

Kama ilivyo kwa dunia, Mars ina majira aina nne lakini kwa saizi ni ndogo ukilinganisha na dunia.

Sayari hii pia ina mlima mkubwa zaidi unaoshikilia nafasi ya pili katika mfumo wa jua unaoitwa Olympus Mons ambao ni mrefu kuliko mlima wowote uliopo duniani. Mlimma huu unaaminika kuwa ulikuwa na volcano lakini kutokana na mabadiliko ndani ya sayari, Volcano hiyo imegeuka kuwa mfu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here