31.3 C
Dar es Salaam
Friday, December 2, 2022

Contact us: [email protected]

Marioo apata dili la ubalozi kampuni ya JCW

Msanii wa bongo Fleva nchini, Omary Ally ‘Marioo’ amepata ubalozi na (JCW)  wamempa gari ambalo litamsaidia katika shughuli zake na tamasha lake  analotarajia kufanya Oktoba 2 mwaka huu mkoani Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Marioo alisema kuwa anashukuru kwa kampuni hiyo ya JCW kwa kuona mchango wake katika tasnia ya muziki na kumwamini kuwa balozi wao.

“Nimekuwa balozi wa JCW wamenipa gari aina ya Land Cruza Prado TX kutokana na jitihada zangu katika muziki, pia Oktoba 2 nitakuwa na shoo yangu nitakayoifanya mkoani Dodoma.

Pia aliongeza kuhusiana na kutaka kujiuwa Marioo amesema kuwa”Siwezi kuacha mikuku minyama ya ngombe halafu nijinyonge siwezi kujinyonga kisa mapenzi bali ni wimbo wangu mpya nilioufanya sina maumivu ya mahusiano bali ni wimbo wangu mpya wa ‘Kitanzi”anasema  Marioo
Miongoni mwa wasanii watakao shiriki kwenye tamasha lao ni Gigy Money, Meja Kunta, Careen,  Hemed Phd pamoja na Wini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,507FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles