25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Mariam Ismail; Sungusungu aliyegeuka staa Bongo Muvi

mariam Ismail
mariam Ismail

NA JOHANES RESPICHIUS,

UNAWEZA kumuogopa utakapomuona akifanya yake kwenye filamu kutokana na kuvaa uhalisia ipasavyo hasa anapoigiza kikatili. Lakini pia anaweza kuigiza sehemu za huzuni vizuri sana.

Anaitwa Mariam Ismail, staa huyu wa filamu za Kitanzania, amefanya vema kwenye filamu nyingi zikiwemo ‘Mr Kadamanja’ akiwa ameshirikishwa na Steven Charles Almas na marehemu Adam Kuambiana na Danija ambayo amecheza kama mke wa Jacob Steophen ‘JB’.

Tumemdondosha mkali huyu ili kufahamu mengi ambayo huenda ulikuwa huyafahamu kutoka kwake akiwa ndani na nje ya tasnia ya filamu. Fuatilia…

MY STYLE: Nje ya sanaa, wewe ni mtu wa aina gani?

MARIAM: Mimi napenda sana sana maendeleo na nina ndoto ya kufika mbali kimaisha.

MY STYLE: Ratiba yako ya siku huwa unaipangilia vipi?

MARIAM: Ni ya kawaida lakini mara nyingi huwa inapangwa na management yangu kwahiyo nikija kuanza siku yangu nakuwa najua shughuli ya kufanya na inanilazimu kuitimiza kama ilivyopanga… kifupi sina  ratiba maalum.

MY STYLE: Tofauti ya Marium wa kwenye runinga na wa nyumbani ni ipi?

MARIAM: Tofauti ipo na ni kubwa sana kutokana na nikiwa nyumbani nakuwa kama dada wa kawaida lakini nikiwa kwenye kazi huwa nakuwa serious.

MY STYLE: Najua hujaolewa bado, mwanaume wa kukuoa anatakiwa kuwa na sifa zipi?

MARIAM: Awe mcha Mungu, mwenye upendo na anisikilize kama mke wake.

MY STYLE: Unatumia gharama kiasi gani ukiingia salon kuanzia nywele mpaka kucha za miguu?

MARIAM: Inategemea na aina ya nywele ninayotaka kuweka… mara nyingi huwa napenda kuwa natural, yaani kuwa na nywele zangu halisia, ila siku nikiweka nywele natumia si chini ya 400,000, kucha ni 70,000.

MY STYLE: Mara ya kwanza kucheza scene ya kukiss ulipata ugumu gani?

MARIAM: Kiukweli sikiwahi kuona ugumu wowote kwa sababu hiyo ni kazi yangu niliyoamua kufanya, hivyo lazima nikubiliane na kila linalokuja mbele yangu.

MY STYLE: Inasemekana ni lazima utembee na director ndiyo upewe nafasi kubwa ya kucheza filamu. Hilo unalizungumziaje?

MARIAM: Kwangu halijawahi kunitokea, ila nadhani wanaofanyiwa hivyo wanakuwa wamejilengesha wenyewe ili wapewe u-main character, nadhani hao wanahisi kutembea nao ndiyo watapewa kipaumbele kucheza filamu nyingi na kuwa staa. Namshukuru Mungu William Mtitu alinitoa kutokana na uwezo wangu wa kuigiza na sijawahi kupata kikwazo chochote kwenye kampuni yake.

MY STYLE: Ni skendo au jambo gani limewahi kukupata na huwezi kulisahau?

MARIAM: Sijawahi kupata skendo na wala sizitaki kwani naamini zinaweza kunishushia heshima yangu. Naamini ustaa bila skendo inawezekana.

MY STYLE: Umewahi kuachwa au kuacha na mpenzi wako? Ilikuwaje?

MARIAM: Yote yamewahi kunikuta, kuachwa na kuacha, kwenye mapenzi kuna mambo mengi sana ambayo siwezi kuhadithia, ndiyo maana nikaamua nikae bila bugdha ya mapenzi, najaribu kujiweka mbali sana na mapenzi.

MY STYLE: Jambo gani hujawahi kulisema sehemu yoyote na unadhani inaweza kuwa wakati muafaka sasa wa kuwaambia mashabiki zako?

MARIAM: Mimi asili yangu nusu Mnyarwanda na nusu Mnyamwezi, pia kabla ya kuanza sanaa mwaka 2008 nilikuwa ‘Sungusungu’ eneo la Mbagala.

MY STYLE: Unatumia kilevi gani?

MARIAM: Kutokana na shughuli ninazozifanya siwezi kutaja aina ya kilevi ninachotumia  kwa sababu nitakuwa kama nakipigia promo hicho kinywaji. Lakini kifupi napenda sana Spirits na Gin.

MY STYLE: Mwisho kabisa, una ushauri gani kwa mastaa wanaotumia madawa ya kulevya?

MARIAM: Toka enzi za akina marehemu Amina Chifupa, alipiga kelele nyingi sana kuhusu madawa ya kulevya, wenye kusikia watasikia. Lakini watu wamekuwa wakiendelea kuziba masiko na kuthubutu kuendelea na matumizi ya madawa hayo.

Mimi sidhani kama naweza kuwa na ushauri zaidi, ni wao kuusikiliza na kufanyia kazi kwa sababu kama ni ushauri walishapewa sana na watu mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles