24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Mariah Carey atafuta nguo za harusi

MariahaLAS VEGAS, MAREKANI

NYOTA wa muziki nchini Marekani, Mariah Carey, ameanza kutafuta nguo kwa ajili ya harusi yake itakayofungwa hivi karibuni.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 47, anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake mfanyabiashara, James Packer, raia wa nchini Australia, lakini bado wawili hao hawajaweka wazi harusi hiyo itakavyofungwa.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, mrembo huyo ameweka picha ikimwonyesha akiwa amevaa nguo kama anafunga ndoa pindi alipokuwa akijaribu nguo hizo.

“Muda unakaribia wa kufunga ndoa, kinachofanyika kwa sasa ni kutafuta vazi sahihi kwa ajili ya siku hiyo, najua yapo mengi lakini bado sijalipata linalonivutia,” aliandika Mariah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles