24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MARGARET SITTA ALIA NA KODI KWA WAFANYAKAZI

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


RAIS mstaafu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Margaret Sitta, amesema kwa sasa watumishi wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi, ikiwamo ukubwa wa kodi kwenye mshahara, huku baadhi ya waajiri hawavitambui vyama hivyo.

Hayo aliyasema juzi, jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, ambapo alisema itakuwa ni jambo jema zaidi kama waajiri watakaa na wafanyakazi wao na kuziangalia changamoto zilizopo.

“Serikali na makampuni binafsi hulipa kwa mwezi mishahara duni ambapo ni ujira mdogo sana kwa siku ikilinganishwa na kupanda kwa gharama za maisha.

“Kwa sasa ukubwa wa kodi ya mapato kwa wafanyakazi (PAYE) kodi ya mapato inayotozwa na Serikali inawalazimisha watumishi wa serikali na sekta binafsi kulipa kodi mara tatu na zaidi,” alisema Sitta.

Alisema miongoni mwa ulipaji wa kodi hizo ni pamoja na ulipaji kupitia mishahara yao ya kila mwezi, kulipa kodi kila wanunuapo bidhaa mbalimbali na ulipaji wa kodi wakati wa kustaafu.

Alisema tatizo jingine kubwa ni baadhi ya taasisi za umma na za binafsi ambazo zimekuwa zikikwepa kutekeleza sheria za kazi, ikiwamo sheria ya ajira na mahusiano kazini, sheria Na. 6 ya mwaka 2004.

Rais huyo mstaafu wa Tucta, alisema sheria hiyo inalenga kuwashirikisha wafanyakazi kupitia mabaraza ya wafanyakazi kupitisha bajeti za taasisi za umma zilizopokelewa bungeni bila kuzingatia sheria hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles