MAREKANI YAWAKARIBISHA KOREA KASKAZINI

0
698

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS Donald Trump wa Marekani ameahidi kukamilisha makubaliano ya kuondoa silaha za nyukilia katika Rasi ya Korea, akishirikiana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, hatua inayoashiria kuwa mazungumzo kuhusiana na suala hilo bado yako hai, baada ya wiki kadhaa za mkwamo. Trump ameandika katika ukurasa Twita kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un ana imani isiyoyumba kwa Rais Trump na kumshukuru kiongozi huyo. Ujumbe huo wa Trump katika ukurasa wa Twitter umekuja saa kadhaa baada ya Kim Jong-un kurejelea kauli yake ya kuheshimu na kuhakikisha anatekeleza ahadi yake ya kuondoa silaha za nyuklia katika mazungumzo yake na mjumbe maalumu wa Korea Kusini, kabla ya mkutano wa kilele kati ya Kim Jong-un na Rais wa Korea Kusini uliopangwa kufanyika Septemba 18 hadi 20, mjini Pyongyang.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here