Rais wa Marekani Donald Trump, ametaka mazungumzo na viongozi wa Iran, katika wakati huu ambapo mvutano baina yao unazidi kupamba moto baada ya Trump kuiondoa nchi yake kwenye makubaliano ya nyuklia na taifa hilo la Kiislamu.
Trump amewaambia waandishi wa habari katika ikulu ya White House kuwa yuko tayari kwa mazungumzo na angetaka viongozi wa Iran kumtafuta.
Kauli hiyo ya Trump inakuja ikiwa ni siku chache baada ya kupeleka ndege za kivita na silaha nyingine zenye uwezo wa kufyatua makombora ya nyuklia katika eneo la Mashariki ya Kati, ikisema ina taarifa kuwa kuna mipango ya mashambulizi yatakayoungwa mkono na Iran.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, amesisitiza kuwa Marekani haipo tayari kwa vita.