26.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 26, 2022

MAREKANI YASITISHA MSAADA KWA SEKTA YA AFYA KENYA

NAIROBI, KENYA

SHIRIKA la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo la Marekani (USAID), ambalo hutumiwa na taifa hilo kutoa misaada kwa mataifa ya nje, limesitisha ufadhili wake kwa miradi ya afya nchini Kenya.

Taarifa kutoka shirika hilo imesema hatua ya kusitisha ufadhili kwa miradi yote ya Wizara ya Afya ya Kenya imetokana na hatua ya Kenya kutotimiza masharti ambayo haikuyataja.

Maafisa wa USAID wameagizwa kutojishughulisha na ‘shughuli zozote za kibiashara’ na taasisi za serikali ya Kenya pamoja na mashirika mengine yenye uhusiano na serikali.

Hatua hiyo ya Marekani inatarajiwa kuathiri miradi mbalimbali ya serikali ikiwemo mipango ya kukabiliana na malaria, kifua kikuu na Ukimwi.

Mingine ni miradi ya uzazi wa mpango, huduma za afya kwa wajawazito na watoto.

Kwa miezi kadhaa sasa, wizara ya afya nchini Kenya imekumbwa na tuhuma za ulaji rushwa.

Sekta ya afya Kenya pia ilitatizwa na mgomo wa kitaifa wa madaktari ambao ulidumu kwa siku 100 kuanzia Desemba mwaka jana.

Mwaka uliopita, mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali alisema jumla ya dola milioni 50 za Marekani hazikubainika zilivyotumiwa katika wizara ya afya.

Maafisa wakuu katika wizara ya afya pamoja na jamaa za baadhi ya viongozi wakuu serikalini walidaiwa kuhusika katika kufujwa kwa fedha hizo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
176,803FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles