27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani yakiri ndege yake kutunguliwa na Iran

WASHINGTON, DC, MAREKANI

JESHI la Marekani limekiri ndege yake kutunguliwa na jeshi la Iran ilipokuwa kwenye anga ya kimataifa kkatika eneo la mpaka kati ya Ghuba ya Oman na Uajemi.

Awali vikosi vya kijeshi vya Iran vilidai vimeshambulia ndege ya kijasusi isiyo na rubani katika anga lake.

Vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti tukio hilo dhidi ya ndege isiyo na rubani waliyoiita RQ-4 Global Hawk, kusini mwa Jimbo la Hormozgan.

Jeshi la Marekani awali halikuthibitisha kama ndege yake imeangushwa, huku msemaji akikana taarifa kuwa ndege yao ilikuwa katika anga la Iran.

Tukio hilo limetokea siku kadhaa baada ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani kusema kuwa watapeleka vikosi 1,000 zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati baada ya kutokea mvutano kati ya Marekani na Iran.

Marekani iliishutumu Iran kushambulia kwa mabomu meli za mafuta katika Ghuba ya Oman.

Mzozo huo ulishika kasi Jumatatu wakati Iran iliposema itazidisha kiwango cha urutubishaji madini ya urani kinyume cha makubaliano na mataifa yenye nguvu duniani ya mwaka 2015.

Iran imefikia uamuzi huo baada ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na Marekani.

Msemaji wa jeshi nchini Marekani, awali aliiambia Reuters kuwa ‘hakuna ndege iliyokuwa ikiruka kwenye anga la Iran leo’, lakini hakutaka kuzungumza zaidi.

Mgogoro umekuwepo kati ya nchi hizo mbili tangu mwaka jana wakati Rais Donald Trump alipojitoa katika mkataba wa kimataifa wa mwaka 2015 uliolenga kumaliza mpango wa nyuklia nchini Iran.

Iran iliamua kuacha kutekeleza kile ambacho iliahidi kufanya mwanzoni mwa mwezi Mei na kutishia kuanza kutengeneza tena nyukilia.

Meli na ndege za jeshi zilizotumwa nchini Iran ambazo wafanyakazi wake sio wa dharura wametakiwa kuondoka.

Siku ya Jumatatu, mkuu huyo wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA), Yukiya Amano, alithibitisha kuwa Iran imeongeza uzalishaji wa madini ya kutengeneza silaha.

Lakini alikataa kutoa maelezo zaidi kuhusu suala hilo japo aliongeza kuwa hawajabainisha ikiwa madini iliyozalisha kufikia sasa imepita kiwango kilichowekwa.

Aliiambia bodi ya usimamizi ya IAEA ni vyema Iran ihakikishe inatekeleza mkataba wa kimataifa wa nyukilia kikamilifu.

Wakati viongozi kutoka pande zote mbili wamesisitiza kuwa hawataki vita itokee, bado mvutano ni mkubwa.

Wanadiplomasia kutoka Marekani wametoa tahadhari kuhusu ndege za kibiashara ambazo zinaenda katika maeneo hayo kuwa ziko hatarini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles