MAREKANI YAKATIZA UFADHILI MPANGO WA UZAZI

0
394

NEW YORK, MAREKANI


SERIKALI ya Marekani imesitisha ufadhili kwa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya Watu (UNFPA) unaotoa msaada kwa ajili ya mpango wa uzazi duniani.

Hatua hiyo italifanya shirika hilo kupoteza takriban dola milioni 30 za ufadhili kwa mwaka huu pekee.

Linakuwa shirika la kwanza la Umoja wa Mataifa kukabiliwa na kupungua kwa ufadhili baada ya ahadi ya kupunguza msaada wa kifedha kutoka kwa utawala wa Trump.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inasema kuwa uamuzi huo ulizingatia shughuli za UNFPA za mpango wake wa uzazi na Serikali ya China, ambazo inasema ulisaidia kutoa mimba na kufunga uzazi kwa lazima.

Badala yake ufadhili huo utaelekezwa katika mipango mingine ya uzazi katika nchi zinazoendelea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here