24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani, Taliban wakubaliana kumaliza uhasama

DOHA- QATAR

MAREKANI na kundi la Taliban wamesaini mkataba wa makubaliano unaolenga kuwezesha kupatikana kwa amani ya kudumu Afghanistan baada ya mapigano ya zaidi ya miaka 18.

Pia Marekani na washirika wake Umoja wa Kujihami (Nato) wamekubaliana kuondoa wanajeshi wake katika taifa hilo kwa muda wa miezi 14, kama wanajeshi watadumisha mkataba huo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo na kiongozi wa Taliban walihudhuria hafla ya utilianaji saini mkataba huo katika hafla iliyofanyika mjini wa Doha, Qatar jana.

Baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo mazungumzo kati ya serikali ya Afghanistan na kundi la Taliban yatafuata ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano hayo.

Kupitia makubaliano hayo wanamgambo wa Taliban pia wamekubaliana kuruhusu kundi la al-Qaeda na makundi mengine yenye msimamo mkali kufanya shughuli zao katika maeneo wanayoyadhibiti.

Marekani ilivamia Afghanistan tangu mwaka 2001 na zaidi ya wanajeshi 2400 wa Marekani wameuwawa katika mapigano hayo, huku wengine zaidi ya 12,000 wakiendelea kuhudumu katika taifa hilo. Kupitia makubaliano hayo Rais Trump wa Marekeani amehaidi kumaliza uhasama huo wa muda mrefu. Kuanzia mwaka  2011, Qatar imekuwa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles