Doha, Qatar
KATIKA kikao kilichozikutanisha Marekani na Taliban huko Qatar, taifa hilo lenye nguvu ya kiuchumi duniani limekubali kusambaza misaada ya kibinadamu nchini Afghanistan.
Pande mbili hizo zimekaa mezani kwa mara ya kwanza tangu Taliban ilipoingia madarakani Agosti, mwaka huu, hatua hiyo ikija baada ya Marekani kuondosha wanajeshi wake Afghanistan.
Mbali ya ‘ishu’ ya misaada, pia mazungumzo yao yalijadili namna Afghanistan itakavyolindwa dhidi ya vikundi vya kigaidi vilivyoko ndani ya nchi hiyo.
Kwa upande wao, maafisa wa Marekani waliyataja mazungumzo kwenda kiweledi, huku wakisisitiza kuwa ni zamu ya Taliban kuonesha kwa vitendo dhamira yao ya kutelekeza yale yaliyojadiliwa.