27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAREKANI: MAKUBALIANO YA NYUKLIA NA IRAN YA UONGO

WASHINGTON, MAREKANI



WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo anasema makubaliano muhimu na Iran ya nyuklia yalitokana na uongo, baada ya Israel kudai kwamba ina ushahidi kuhusu mpango wa siri wa nyuklia wa Iran.

Amesema inadhihirisha makubaliano hayo ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani mwaka 2015, yalitokana na uongo na si nia njema.

Rais Trump ameashiria kwa muda mrefu azma yake ya kujitoa katika makubaliano hayo na anatarajiwa kutoa uamuzi katika wiki chache zijazo.

Mapema wiki hii, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu aliishutumu Iran kwa kuendeleza mpango wa kuunda zana za nyuklia kupitia mradi uliopewa jina ‘Project Amad’.

Amesema nchi hiyo imeendelea kujifunza kuhusu kuunda silaha za nyuklia baada ya awali mradi huo kusitishwa mwaka 2003.
Hilo lilifuata ufichuzi wa mwaka 2002 wa kundi la upinzani linaloishi uhamishoni lililosema Iran inaunda maeneo ya siri ya urutubishaji nyuklia kinyume na makubaliano ya nyuklia ambayo Iran ilitia saini kuyatii.

Netanyahu aliwasilisha kile alichokitaja kuwa ushahidi wa maelfu ya nyaraka za siri za nyuklia zilizoonyesha kuwa Iran ilidanganya kuhusu azma yake ya kuunda zana za nyuklia kabla ya makubaliano hayo muhimu yalioidhinishwa mwaka 2015.

Lakini Iran imekuwa ikikana kuunda zana za nyuklia, na ilikubali miaka mitatu iliyopita kusitisha mpango wake wa kuunda nishati ya nyuklia ili iondolewe vikwazo.

“Nyaraka zilizopatikana na Israel kutoka ndani ya Iran zinaonyesha pasi na shaka kuwa utawala wa Iran ulikuwa hausemi ukweli,” Pompeo alisema katika taarifa yake.

“Tumekagua nyaraka tulizoziona ni za kweli, “alisema akiongeza: “Iran ilificha mpango mkubwa wa nyuklia dhidi ya dunia na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) – mpaka leo.”
Pompeo pia alionya kwamba Marekani sasa “inakagua ufichuzi huo wa nyaraka za siri wa Iran una maana gani kwa siku zijazo”.

Trump, ambaye alizungumza wazi kuhusu upinzani wake wa makubalian hayo na Iran yaliyofikiwa wakati wa utawala wa Rais Barack Obama, amesema ametizama sehemu ya aliyowasilisha Netanyahu, akisema hali hiyo haikubaliki.

Amesema atafanya uamuzi kuhusu iwapo aendelee kushikilia makubaliano hayo siku au kabla ya Mei 12.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles