25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani kuzidi kuzibana nchi zinazonunua mafuta Iran

NEW YORK, Marekani

SERIKALI ya nchi hii  huenda ikayawekea vikwazo mataifa matano ambayo yanaendelea kununua mafuta kutoka   Iran

Mataifa hayo ni  pamoja na washirika wake Japan, Korea Kusini na Uturuki iwapo yataendelea kununua mafuta kutoka   nchi hiyo.

 Maofisa watatu wa serikali walisema juzi kuwa  Waziri wa Mambo ya Nje,  Mike Pompeo, anatarajiwa kutangaza  kwamba serikali yake haitaongeza muda wa kuondolewa kwa vikwazo kwa mataifa hayo matano vitakapofikia muda wake wa mwisho Mei 2 mwaka huu.

Walisema  mataifa mengine yanayokabiliwa na kitisho hicho ni China na India.

Hata hivyo haikuwekwa wazi iwapo miongoni mwa mataifa hayo matano yatapewa muda zaidi wa kumalizia ununuzi ama watakabiliwa na vikwazo hivyo vya Marekani vitakavyoanza Mei 3 kama hawatasimamisha mara moja kuagiza bidhaa hiyo kutoka Iran.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles