30 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 25, 2022

‘MAREKANI’ KUMSAIDIA RAILA URAIS 2017

WASHINGTON, MAREKANI


SHIRIKA lisilo la kiserikali lenye makao makuu nchini hapa lilikutana na kiongozi wa upinzani nchini hapa, Raila Odinga kujadili jinsi muungano wa upinzani wa NASA nchini Kenya unavyoweza kushinda uchaguzi mkuu ujao.

Shirika hilo, Vanguard Africa, lilibuniwa na mtaalamu mkuu wa kampeni nchini Marekani na lilishatoa ushauri wa kisiasa kwa Odinga wakati wa mkutano wao mjini Washington,  kwa mujibu wa barua iliyohifadhiwa katika Wizara ya Sheria Marekani.

“Tunatarajia kuwa na mazungumzo zaidi shirikishi na ya wazi kuhusu kampeni zako, changamoto za sasa na uwezekano wa kupata ushindi,” inasema barua hiyo kwenda kwa Raila kabla ya mkutano wao.

Maafisa hao wanaongeza kwamba wanalenga kampeni za upinzani ulioungana ili kuimarisha nafasi ya kupata ushindi.

“Tunahisi muungano wa upinzani unakupatia nafasi ya kupata ushindi katika uchaguzi na kuendeleza rekodi yako kama kiongozi mashuhuri barani Afrika,” maofisa wa Vanguard wanasema katika barua hiyo.

Mwaliko kwa Odinga kukutana na vigogo wa shirika hilo ulitolewa kwa mujibu wa sheria za Marekani zinazohitaji mashirika kufichua kazi wanayofanya kwa niaba ya serikali na wanasiasa katika mataifa mengine.

Katika barua hiyo, Vanguard Africa walieleza jinsi walivyousaidia muungano wa upinzani kupata ushindi nchini Gambia na hivyo kumweka madarakani Rais wa sasa Adama Barrow.

Kwa sababu hiyo, Vanguard Afrika inahisi inaweza kurudia kitendo hicho nchini Kenya”.

Akihojiwa na vyombo vya habari, Mkurugenzi Mkuu wa Vanguard Africa, Jeffrey Smith hakueleza iwapo wanamuunga mkono Odinga kugombea urais.

Alisema Vanguard Africa, linalofadhiliwa na watu binafsi halikupokea fedha kutoka kwa Odinga na kwamba si la mamluki.

Shirika hilo lilisema uamuzi wa kushirikisha na kufadhili wanasiasa nchini Kenya na kote Afrika unatokana na ukweli kuwa wapo baadhi ya viongozi wenye  maono ambao hawana fedha na maarifa ya kushindana kikamilifu na wanasiasa walio madarakani.

Alipoulizwa iwapo Vanguard Africa linaweza kumuunga Rais Uhuru Kenyatta, Smith alisema: “Maoni yangu binafsi ni kwamba yeye si kiongozi tunayeweza kushirikiana naye”.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
176,563FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles