26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani kuliorodhesha Jeshi la Iran kundi la kigaidi

WASHINGTON, MAREKANI

MAREKANI inapanga kuliorodhesha Jeshi la Mapinduzi ya Iran kuwa miongoni mwa makundi ya kigaidi duniani.

Maafisa wawili wa Serikali ya Marekani na Bunge walithibitisha hilo japokuwa hawaruhusiwi kulizungumza hadharani, hivyo waliyasema hayo kwa misingi ya kutotaka majina yao kutajwa.

Marekani, awali iliripotiwa na gazeti la Wall Street la hapa kuwa inapanga kuweka vikwazo mbalimbali ikiwemo kutaifisha mali za jeshi hilo zilizoko Marekani na kupiga marufuku Wamarekani kufanya biashara nalo au kulisaidia kwa njia yoyote ile.

Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Serikali ya Marekani kukiorodhesha kikosi cha jeshi la nchi nyingine kuwa miongoni mwa makundi ya kigaidi.

Hata hivyo, serikali zilizopita za Marekani zilikuwa zimekilenga kikosi kingine cha Iran cha Quds kuwa miongoni mwa makundi ya kigaidi.

Waziri wa Masuala ya Kigeni wa Iran, Javad Zarif katika ujumbe alioandika kwenye mtandao wa Twitter akimlenga Rais wa Marekani, Donald Trump alisema anapaswa kutafakari kwa kina anapofanya maamuzi kuliko kuitumbukiza Marekani katika janga jingine.

Jeshi la Mapinduzi ya Iran lina udhibiti mkubwa na ushawishi katika uchumi wa Iran hivyo vikwazo vya Marekani dhidi yake havina athari kubwa kwake.

Hata hivyo, vitatatiza kwa kiasi kikubwa masuala kijeshi na ya kidiplomasia ya Serikali ya Marekani hasa nchini Irak, ambako makundi mengi ya wanamgambo wa Kishia na vyama vya siasa vina uhusiano wa karibu na kikosi hicho.

Aidha kwa hatua hiyo, nchini Lebanon itakuwa Marekani imejiongezea vizuizi yenyewe na kushindwa kujua afisa yupi wa kushirikiana naye kwa sababu jeshi hilo lina mafungamano na Hezbollah kundi ambalo ni sehemu ya serikali ya Lebanon.

Tayari Marekani imelilenga Hezbollah kuwa kundi la kigaidi na uwepo wake katika Bunge na Baraza la mawaziri la Lebanon kumeilazimisha Marekani kuiepuka serikali ya Lebanon japokuwa inaendelea kuisaidia na kufanya kazi na jeshi la Lebanon.

Aidha taasisi mbali mbali za Marekanii hazijapokea vyema wazo hilo.

Wizara ya ulinzi na taasisi za ujasusi nchini hapa zimeonyesha wasiwasi wao juu ya athari ya uamuzi huo vikijiuliza iwapo hatua hiyo haitawaruhusu kuwasiliana na maafisa wa kigeni waliowahi kushirikiana au kuwasiliana na wakuu wa vikosi hivyo vya mapinduzi.

Wasiwasi huo ndio kwa kiasi kikubwa ulizuia Serikali zilizopita za Marekani kuchukua uamuzi, ambao umekuwa ukifikiriwa kwa miongo kadhaa sasa.

Afisa mwingine wa Serikali ya Marekani, ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema makamanda wa jeshi la Marekani pia wameingia wasiwasi kwa hatua hiyo kuwa inaweza kuifanya Iran nayo kulipiza kisasi kwa kuviwekea vikwazo vikosi vya Marekani vilivyobakia Irak, Syria, na kwengineko. Maofisa hao kwa sasa wanapanga kuitahadharisha Marekani juu ya hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles