24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

MAREKANI KIMBILIO LA WANAFUNZI WENGI DUNIANI

Na Joseph Lino,

MAREKANI ni miongoni mwa mataifa yaliyopiga hatua kubwa katika masuala ya elimu ya juu. Wanafunzi wengi kutoka pande zote za duniani ambao wanauwezo wa kwenda kusoma nje, kitu cha kwanza hufikiria ni nchi gani anaweza akapata elimu bora na yenye mafaniko. Kwa upande mwingine vyuo vikuu vya Marekani vinakuwa vya kwanza kufikiriwa.

Takwimu zinaonyesha kuwa Marekani ni miongoni mwa nchi zenye wanafunzi wengi kutoka nje, kwa mfano wanafunzi zaidi ya 900,000 kutoka mataifa mbalimbali walikwenda kusoma nchini humo muhula wa masomo  mwaka 2013/14.

Lakini kitu kikubwa cha kujiuliza hapa ni kwanini wanafunzi wa mataifa ya kigeni wanachagua kwenda kusoma Marekani?

Kuna sababu tofauti ambazo mara nyingi kila mwanafunzi kabla ya kufanya uamuzi wa kuchagua nchi gani anaweza kwenda kusoma, kitu cha kwanza ni lazima aridhike na kiwango cha elimu kinachotolewa katika nchi husika pamoja na fursa zinazoenda sambasamba atakapokuwa huko.

Sababu ya kwanza ni mipango bora ya kielimu: Marekani inajulikana dunia nzima kwa kuwa na vyuo vikuu maarufu ambavyo vinatoa kozi za taaluma mbalimbali. Mwanafunzi mmoja kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins anasema Marekani ina sifa kubwa ya elimu ya juu.

“Kuna masuala mengi katika kuchagua elimu hata njia mbadala ya elimu hapa Marekani ni tofauti na nchi ninayotoka,” anasema.

 Fursa za kazi kwa wenye nia ya kujifunza

Katika nyongeza ya kusoma nchini Marekani, wanafunzi wengi hujiunga na klabu na taasisi kitaaluma zinazohusiana au kutohusiana na taaluma wanazosomea. Taasisi na klabu hizi zinatoa fursa kwa mwanafunzi kujifunza ujuzi ambao anaweza kutumia katika taaluma zao.

Kwa mfano; Chuo Kikuu cha Georgetown kinatoa nafasi kwa wanafunzi wanaosoma taaluma ya uandishi kujiunga na klabu ya chapter of the Society of Professional Journalists (SPJ) kwaajili ya kuwasaidia taaluma zao. Akiwa mwanachama wa klabu hiyo anapata fursa za kuhudhuria mikutano ya waandishi wa habari, kujenga mtandao na uzoefu mbalimbali wa kitaalamu.

 Rasilimali na maktaba maalumu

Vyuo vya Marekani vinatoa ofa rasilimali nyingi  za kuwasaidia katika masomo yao kama vitabu na majarida ya kitaaluma, lakini vyuo vya Marekani mara nyingi hakuna matatizo ya ukosefu wa vitabu wala kutafuta vitabu unavyohitaji ambavyo nchi nyingine ni vigumu kupata.

 Kozi za lugha ya Kiingereza

Vyuo vingi na shule za binafsi hufundisha somo la Kiingereza kama lugha ya pili ili kuwasaidia wanafuzi kuelewa na kusoma lugha hiyo kwa ufasaha.

Wanafunzi wengine wa nje wanaokwenda Marekani huchukua masomo ya Kiingereza kwa lengo la kujiandaa na kujiunga na masomo ya chuo kikuu. Wengine huenda kuzoea maisha ya nchini humo, kuboresha lugha ya Kiingereza au kufanya kazi.

Mwanafunzi wa  Chuo Kuu cha International Language Institute kilichopo Washington D.C, Kang Han anasema  kabla hajaanza mazoezi ya kazi Marekani, alichukua kozi ya lugha ya Kiingereza ambayo ilimsaidia kuweza kuzungumza lugha hiyo kwa ufasaha, kuandika na kusoma, pia ilimsadia kuelewa tamanduni za Wamarekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles