23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani, China zatupiana tena lawama kuhusu janga la Corona

BEIJING, CHINA

VITA vya maneno vinaendelea kati ya Marekani na China, ambapo nchi hizo zimetupiana tena lawama kuhusu janga la virusi vya Corona.

Vuta nikuvute kati ya Marekani na China inaendelea baada ya China kumshtumu Rais Donald Trump wa Marekani kwa kujaribu kuilaumu China kuhusu janga la virusi vya Corona.

Hii ni baada ya Trump mapema Alhamisi wiki hii kusema kuwa dunia inalipa deni kubwa kutokana na ukosefu wa uwazi wa China wakati mlipuko wa virusi vya Corona ulipozuka katika mji mkuu wa Wuhan mwishoni mwa mwaka jana.

China imekosolewa vikali kwa kuficha ukweli kuhusu virusi hivyo na hata kuwaadhibu baadhi ya watu waliofichua siri kuhusu virusi hivyo mwanzoni kabisa vilipotokea.

Kwa mujibu data za shirika la habari la AFP, ugonjwa wa COVID-19 umewaua karibu watu 10,000 huku wengine 232,000 wakiambukizwa virusi vya Corona kote duniani.

Rais wa jimbo la Lombardy, nchini Italia, Attilio Fontana ameitaka serikali kukaza kamba zaidi na kuhakikisha vikwazo vilivyowekwa vinatekelezwa. 

Bila kutaja idadi, Fontana amesema kuwa virusi vya corona vinaendelea kuenea kwa kasi katika jimbo hilo ambalo limerekodi maambukizi mengi na hata vifo kuliko majimbo yote nchini Italia.

Aidha vilabu vya soka, wachezaji na hata mashabiki wa mpira nchini humo wameungana ili kuchangisha fedha kwa ajili ya kuusaidia mfumo wa afya nchini humo ambao unaonekana kulemewa na mlipuko wa virusi vya corona.

Nchini Iran, viongozi nchini humo wameapa kuibuka na ushindi katika mapambano dhidi ya mlipuko wa corona. Viongozi hao wametoa ujumbe wa kuwatia moyo raia wake wakati huu ambapo jana waliadhimisha sikukuu ya mwaka mpya wa Iran.

Naibu waziri wa afya nchini Iran Alireza Raisi amesema: “Idadi ya watu waliopona imefika 6,745. Hata hivyo, watu wengine 149 walikufa jana na hivyo kufikisha jumla ya watu 1433.

Nchini Ujerumani, msemaji wa wizara ya fedha Denis Kolberg amesema kuwa serikali itafanya kila iwezalo kuusaidia uchumi wake hasa wakati huu ambapo janga la Corona linaendelea kuutikisa uchumi wa Ulaya.

Kolberg ameongeza kuwa Ujerumani inafanya mazungumzo na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya juu ya njia za kupunguza athari ya kiuchumi na kuwa Ujerumani iko tayari kuunga mkono utoaji wa dhamana za pamoja za mataifa yanayotumia sarafu ya Euro.

Kwa upande wa Hispania, waziri wa Afya Salvador Illa amesema jeshi litasaidia kuweka vitanda 5,500 pamoja na kuboresha huduma ndani ya kituo maalum cha matibabu mjini Madrid. 

Pia hoteli mjini humo zimeanza kugeuzwa kama hospitali hasa kwa wagonjwa wenye mahitaji ya dharura. 

Mjio huo umerekodi zaidi ya maambukizi 7,000 ya virusi vya corona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles