26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

Marekani: China itasema ilikotoa Corona

RAIS wa Marekani, Joe Biden, amesema Serikali yake
itaendelea kuikaba koo China hadi nchi hiyo ya Asia ianike
chanzo cha janga la Corona.

China imekuwa ikinyooshewa kidole kwa madai ya kuwa
chanzo cha Corona ikielezwa kuwa virusi vya ugonjwa huo
vilitoroka katika maabara zake.

Marekani inaamini China haitoi ushirikiano wa kutosha
katika jitihada za kubaini chimbuko la Corona lakini
itaendelea kuishinikiza hadi pale itakapokubali.

“Taarifa nyeti juu ya chimbuko la hili janga zinapatikana
China lakini tangu mwanzo viongozi wa Serikali wamekuwa
hawataki wachunguzi wa kimataifa wazipate,” amesema
Biden.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,740FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles