25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Marehemu aonekana mtaani akiwa hai

JENEZANa Ibrahim Yassin, Mbarali

WAKAZI wa Kijiji cha Warumba, Kata ya Imalilo Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, wamejikuta katika hali ya sintofahamu baada ya kumwona mtu anayedaiwa kufariki dunia Agosti 24, mwaka huu akitembea mtaani.

Mtu huyo, John Yonga (29) anadaiwa kuonekana sehemu mbalimbali za kata hiyo akiwa hajavaa nguo isipokuwa shanga nyekundu kiunoni, huku tukio hilo likihusishwa na ushirikina.

Baba mzazi wa marehemu huyo, Exavery Yonga alisema kabla ya kufariki mwanawe aliugua na kupelekwa katika Zahanati ya Madibila, ambapo hali ilizidi kuwa mbaya ndipo alipofariki dunia wakati akipatiwa matibabu.

“Alifariki Agosti 24 na tukazika kesho yake Agosti 25, mwaka huu katika Kijiji cha Warumba. Najua mwanangu amefariki, lakini nasikia ameanza kuonekana kuanzia Agosti 31 mwaka huu katika maeneo mbalimbali akiwa hai ila mimi sijamwona nimeletewa taarifa tu za kuonekana kwake,” alisema.

Baadhi ya mashuhuda waliokutana na marehemu huyo walisema amekuwa akionekana akiwa mtupu na wakati mwingine akiwa na nguo au shanga katika maeneo tofauti.

“Ni John (marehemu) kabisa, yule tunajua alifariki na kuzikwa lakini tunashangaa anaonekana mtaani akiwa haongei chochote hata ukimwongelesha,” alisema mmoja wa wakazi hao Tabu Nassoro.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Warumba, Ajuta Kitaule, alikiri kupata taarifa za uwepo wa mtu huyo aliyefariki dunia na amekuwa akionekana mitaani akiwa hai.

“Nimesikia taarifa hizo kwa watu kwa kweli kama serikali hatuna namna ya kufanya kwa kuwa serikali haiamini mambo ya kishirikina, hivyo nawaomba wananchi kuwa watulivu kwa kuwa tukio hilo ni la kwanza kutokea kijijini hapa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles