26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

MARAIS WAWILI NCHINI COMORO WAHUSISHWA KASHFA YA PASIPOTI

MORONI, COMORO


MARAIS wawili wa zamani wa Comoro, Ahmed Abdallah Mohamed Sambi na Ikililou Dhoinine, wanashukiwa kuhusika na ubadhirifu wa mamilioni ya Dola za Marekani kwa kuuza pasipoti kwa wageni wa mataifa mawili ya Ghuba.

Kwa mujibu wa ripoti ya Bunge, mahakama imetakiwa ichukue jukumu la kushughulikia matukio hayo ya ubadhirifu wa fedha za umma na kula njama ambayo marais hao wawili wa zamani wamehusishwa.

Kashfa hiyo inaanzia nyuma mwaka 2008 wakati Comoro ilipoanzisha mpango kwa kushirikiana na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Kuwait, kuwapa uraia wakazi wa mataifa hayo mawili jamii ya Mabedui ambao hawatambuliwi kuwa na utaifa wa nchi yoyote.

Badala yake, Comoro ilitarajiwa kupokea vitega uchumi muhimu kutoka mataifa hayo yenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Makubaliano ya awali ni kwamba familia 4,000 za Mabedui zingepewa uraia wa Comoro na visiwa hivyo kulipwa Dola za Marekani milioni 163, ambazo zingetumiwa katika miradi ya miundombinu.

Miaka iliyofuata, karibu hati 48,000 za kusafiria zilitolewa, lakini kwa mujibu wa uchunguzi wa Bunge, ni pasipoti 6,000 tu walizopewa Mabedui, lakini pia zikiuzwa nje ya utaratibu.

Ripoti imesema hati hizo ziliuzwa kimagendo, huku mpwa wa Sambi akichapisha pasipoti nyingi kadiri atakavyo kwa mkataba na kampuni moja ya Ubelgiji.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Bunge, sehemu kubwa ya malipo ya pasipoti kati ya 25,000 na 200,000 yaliibwa.

Kwa jumla sehemu kubwa ya fedha hazikuonekana kwenye hazina ya Serikali.

Serikali inakadiriwa imepoteza hadi Dola za Marekani milioni 971, karibu 80 asilimia ya jumla ya pato la taifa.

Rais Sambi, ambaye anadaiwa alipokea kiinua mgongo cha hadi Dola za Marekani milioni 105 kwa kusaini mkataba huo, amekana tuhuma hizo kama ilivyo kwa mrithi wake wa urais, Dhoinine.

Mradi huo wa pasipoti kwa vitega uchumi, sasa umesimamishwa na Rais Azali Assoumani mara tu aliposhinda uchaguzi mwaka 2016.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles