24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Marais wastaafu wakacha sherehe Dodoma

Benjamin Mkapa
Benjamin Mkapa

NA JONAS MUSHI, DAR ES SALAAM

RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume hawakuonekana katika sherehe za makabidhiano ya Katiba inayopendekezwa zilizofanyika jana mjini Dodoma.

Kutokuwapo kwao katika sherehe hizo, kunakwenda tofauti na tangazo lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi aliyesema viongozi wote wastaafu wamealikwa na watakuwapo.

Pamoja na kutokuwapo kwa viongozi hao, haikutolewa taarifa yoyote hadi mwisho wa shughuli hizo.

Mbali na Mkapa na Karume, pia wajumbe wote wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba hawakuwapo katika sherehe hizo.

Kutokana na hali hiyo pia Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, naye kuwepo katika sherehe hizo.

Kutoonekana kwa vigogo hao huenda kukaibua mjadala mzito kwa wananchi kutokana na uzito wa tukio la jana la kukabidhiwa Katiba inayopendekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

- Advertisement -

Related Articles

10 COMMENTS

 1. Ni wazi inajulikana hata kwa Rais na serikali yake kwamba katiba imepitishwa kwa nguvu, na imekataliwa kabisa. Ni mtu gani mwenye akili timamu na busara anaweza kuhudhuria sherehe za katiba haramu? Mabalozi wa mataifa makubwa kama Amerika, Ujerumani, Uingereza walikacha, Maaskofu wa madhehebu yote walikacha, wakawatuma kwa huruma mapadre na wachungaji, Warioba kakacha na tume yake, sasa unafanya sherehe ya kupokea katiba gani? Ni katiba ya CCM walikabidhiana wenyewe, katiba ya wananchi bado haijaanza kujadiliwa, tunaisubiri bado. Mabavu ya Chenge na Sitta yamezaa mgogoro mkubwa wa kikatiba nchini Tanzania. Kikwete asipoangalia ataiacha nchi katika machafuko, mauaji, na vurugu kubwa, yeye ndiye atakayewajibika kwa hilo. Viongozi wa makabisa hawawezi kushiriki uovu wa kubariki katiba haramu, watapona kwa waumini wao? Ni kiongozi gani wa Kikristo mpuuzi anaweza kwenda Dodoma? Hilo wamelikoroga, watalinywa, watanzania wajiandae kwa kura ya hapana, bila kogopa vitisho vya polisi na usalama wa taifa. Kila ktu kina mwanzo na mwisho wake amina. Na CCM ndo inaelkea mwishoni, uwongo hauwezikushinda hata siku moja. Huwezi kuua ukweli hata siku moja . Waliomwua Yesu walifikiri wameshinda kumbe walishindwa kabisa. Hivi ukweli juu ya katiba ya wananchi iutashinda, ushabiki hauna nafasi katika Tz ya leo.

 2. Watanzania tusifikiri hata siku moja kuwa tutakuja kupata malaika wa kutuandikia katiba. Wale wenye mawazo potofu juu ya katiba iliyopendekezwa wasidhani ndiyo maoni ya watanzania.Kama walishindwa kushindana kwa hoja ndani ya bunge la katiba wakaamua kutoka nje ni wazi kuwa hawaitakii mema nchi yetu. Uamuzi wa mwisho juu ya hatma ya katiba iliyopendekezwa uko mikononi mwa watanzania na sio mikononi mwa wale wanaoipinga. Kura ya maoni ndiyo itasema. Haitatokea hata siku moja watu wakakosa kutofautiana maana wengine wana tabia ya kupinga kila kitu ili kupata umaarufu.Watanzania tujiandae na kura ya maoni na tuachane na porojo kuwa katiba inayopendekezwa ni ya CCM. Tusome kwa makini yale yaliyomo ili tuweze kufanya uamuzi sahihi siku ikifika.

  • JOSEPH, HUJAMBO MPENDWA?
   MM NIMEKUSOMA KATIKA MAONI YAKO ILA NIKUKUMBUSHE KUWA KATIBA NI TUNDA LA MARIDHIANO NA SIYO UBABE NA KAA UKIELEWA KUWA URAIS NI TAASISI AMBAYO IKILETA MACHAFUKO KWA KUKIUKA MISINGI YA UTAWALA BORA KUNA MAHAKAMA YA KIMATAIFA IMAMNGOJEA HUYO JK.

   PIA USISAHAU KUWA HATA WABUNGE WA AFRICA MASHARIKI WALICHAGULIWA KIMIZENGWE ILI CHADEMA WASIPATE MBUNGE HATA MMOJA JE UNAJUA KILICHOTOKEA AU UNAFUATA UPEPO?

   NINA MASHAKA NA ELIMU YAKO, UWEZO WAKO WA KUCHAMBUA MAMBO, NA HALI YAKO YA KIMAISHA AMBAYO HUENDA IKAKUFANYA USITATHMINI KABLA YA KUONGEA KWA SABABU NI LAZIMA UWE NA AFYA NJEMA YA AKILI ILI UWEZE KUJADILI HOJA.

   NIKUPE POLE MAANA HUJUI TAIFA LITOKAKO NA HATIMA YETU KWA MAZINGIRA YA SASA.

   MWISHO, UMEONA JOSEPH BUTIKU CCM NO.1 ANACHOSEMA KUHUSU CCM NA SERIKALI YAKE?

   WE LALA TU USINGIZI

 3. Kama dereva wa serikali anatakiwa awe na elimu ya walau kidato cha nne,Je! Kiongoz mbunge yeye ajue kusoma na kuandika tu na achaguliwe sababu ya hela au upendo wake kwa watu na huyo huyo asiye na elimu awe waziri hahahahaaaaaa

  Walau wangetenganisha hapo ni hatari kumuweka waziri asiye na elimu ya International politics and economics afu atuingize tena kwenye mikataba ya ajabu. Mimi kura yangu ni HAPANA ila msinifanye kama AG!

 4. Ni mtanzania gani asiyejua kuwa katiba hii ni ya maccm au na ww ni mjawapo.Sisi tunazungumzia kuachwa kwa maoni ya wananchi ww unaleta habari za waliotoka, hiyo katiba yenu haitapita kwa sababu ni haramu.

 5. Biblia inasema heri mwisho mwema kuliko mwanzo. Wanakoelekea CCM wanafikia mwisho hata kama walianza vizuri sasa hali ni mbaya. Watakaoleta machafuko nchi hii ni watawala wenyewe, Mh Kikwete asipokuwa mangalifu akaendelea kuwasikiliza wapambe wake wanaompa ushauri mbaya lakini asiupime, ataiacha inchi kwenye hali mbaya na yeye atawajibika mbele za Mungu.

  • Fikra za vigogo wa CCM ni kwamba wajukuu na watoto wao watawala watanzania miaka ijayo ndiyo maana wanatengeneza katiba za kuziba wasio wao wasipate nafasi ya kupenya.Nashindwa kuelewa namna gani mtu kama Sitta anasema na kujisifu ni Mzalendo na mwadilifu KAMA KWELI ANAWEZA KUONGOZA WATU KUFUTA UWAZI,UWAJIBIKAJI,UZALENDO kwenye katiba.Najiuliza pia uwezo kiakili na roho zao kama binadam wa watu ambao wanakubaliana na hiyo inayoitwa katiba pendekezi.Nashindwa kuelewa lakini ni vema tutafakari utu wa hawa watu ukizingatia hali halisi ya wizi na ufujaji mkubwa wa rasilimali zetu.Watu wanakuwa kama vile walikuja duniani kumaliza wenzao yaan wana hati miliki na maisha na roho za watu.WATANZANIA TUSIWE WANAFIKI,TUWE WAKWELI KUFUTA UADILIFU,UWAZI,UWAJIBIKAJI,UZALENDO NA MAADILI YA VIONGOZI NI ISHARA YA DHARAU ILIYOKUBUHI,UBABE NA KUFIKRI KUWA KUWA RAIS,WAZIRI,MBUNGE N.K BASI WEWE SHERIA MBOVU UITUNGAYO HAIWEZI KUKUGUSA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles