26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

MARAIS WA KOREA MBILI KUKUTANA LEO

SEOUL, KOREA KUSINI


MARAIS Moon Jae-in wa Korea Kusini na Kim Jong-un wa Korea Kaskazini, wanatarajiwa kukutana nchini hapa leo katika mkutano wa kihistoria baina ya nchi hido mbili ndugu.

Mkutano huo unatarajia kufanyika kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili upande wa Kusini.

Hilo likitokea, Kim atakuwa kiongozi wa kwanza Korea Kaskazini kuingia nchini Korea Kusini tangu kumalizika vita vya Korea mwaka 1953.

Mazungumzo hayo ya kihistoria yatalenga nia ya hivi karibuni ya Korea Kaskazini ya kuachana na silaha za nyuklia.

”Ugumu uko kwenye kufahamu ni kwa kiasi gani watafikia makubaliano kuhusu utayari wa kuachana na silaha za nyuklia,” alieleza msemaji wa Rais wa Korea Kusini, Im Jong-seok.

Mkutano huo wa tatu baada ya mikutano ya mwaka 2000 na 2007, ni matokeo ya jitihada zilizofanyika miezi kadhaa kuimarisha uhusiano kati ya Korea hizi mbili na kufungua milango ya mkutano mwingine wa kihistoria kati ya Kim na Rais wa Marekani, Donald Trump baadaye katika nusu hii ya kwanza mwaka huu.

Kim alitangaza wiki iliyopita kuwa angesitisha majaribio ya silaha za nyuklia, hatua ambayo ilikaribishwa na Marekani na Korea Kusini kama jambo zuri.

Hata hivyo, watafiti wa China wameonyesha kuwa eneo lilikofanyika jaribio la nyuklia la Korea Kaskazini huenda lisitumike tena baada ya mwamba kuporomoka kufuatia jaribio la mwisho Septemba mwaka jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles