29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

MARADONA: ARGENTINA BILA MESSI HAKUNA KITU

BUENOS AIRES, ARGENTINA


NYOTA wa zamani wa timu ya Taifa ya Argentina, Diego Maradona, ameweka wazi kuwa timu hiyo bila ya mshambuliaji wao, Lionel Messi, inaweza ikashindwa kufuzu Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Messi ambaye anakipiga katika klabu ya Barcelona, amefungiwa michezo minne kuitumikia timu yake ya Taifa kutokana na utovu wa nidhamu aliouonesha kwa mwamuzi wa pembeni katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwezi uliopita.

Hadi sasa tayari mchezaji huyo ametumikia mchezo mmoja kutokana na adhabu hiyo, huku akiwa amebakiwa na michezo mitatu, hivyo Maradona amesema timu hiyo ya Taifa itakuwa na wakati mgumu bila ya mchezaji huyo kwa michezo yake iliyobaki.

“Ninayo heshima kubwa katika timu ya Taifa ya Argentina kutokana na kile ambacho nimekifanya kwa miaka ya nyuma, lakini kwa sasa Messi amekuwa na mchango mkubwa ndani ya timu ya Taifa na klabu yake.

“Lakini kuelekea kufuzu Kombe la Dunia mwakani, Messi anatakiwa kukosa michezo minne na tayari amekosa mmoja, ila uwepo wake ndani ya kikosi hicho ni jambo muhimu sana kwa hatua hii.

“Ukweli ni kwamba bila yeye Argentina inaweza kuwa na wakati mgumu sana wa kufuzu kushiriki michuano hiyo mwakani, mara zote tumekuwa tukifanya vizuri, lakini safari hii inaweza kuwa historia.

“Lakini ninaamini Argentina ina kikosi kipana, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa wachezaji waliopo kuonesha ushirikiano wa dhati kuhakikisha timu yao inafuzu michuano hiyo mikubwa duniani.

Michezo ambayo Argentina wamebakisha ili kuweza kufuzu ni pamoja na Uruguay, Venezuela na Peru, michezo hiyo yote Messi ataikosa, lakini atakuwa tayari kucheza katika mchezo wa mwisho dhidi ya Ecuador ambao utapigwa Oktoba 10, mwaka huu.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles