29.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Maradona ajitoa kuifundisha Dorados

CULIACÁN, MEXICO

KOCHA wa timu ya Dorados, Diego Maradona, amejitoa kuifundisha timu hiyo inayoshiriki Ligi daraja la pili nchini Mexico huku akidai kuwa na matatizo ya kiafya.

Kocha huyo raia wa nchini Argentina, hajamaliza mwaka mmoja tangu ateuliwe kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, lakini ameripotiwa kuwa na tatizo la goti pamoja na bega.

Kutokana na hali hiyo, kocha huyo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa bega na goti kwa siku za hivi karibuni, hivyo ameamua kuachana na timu hiyo kwa ajili ya kufanya maandalizi ya matibabu.

Mbali na tatizo la afya, kocha huyo alianza kuonesha dalili za kutaka kuondoka kwa siku za hivi karibuni baada ya kuweka wazi kuwa, kama hatopewa fedha kwa ajili ya kusajili pamoja na kupewa uhuru wa kufanya kazi ataondoka, lakini sasa anaondoka kutokana na tatizo la afya.

“Ukweli tumeishangaza dunia. Tumeonesha kuwa soka ni kitu kinachofanya vizuri kwa watu kujituma kutoka moyoni, asante sana kocha kwa kila ulilolifanya kwetu, tunakutakia kila la heri na tunaamini utapona mapema sana,” waliandika kwenye ukurasa wa Twitter wa timu hiyo.

Maradona mbali na kufanya kazi na timu hiyo, aliwahi kufundisha timu zingine mbalimbali ikiwa pamoja na timu ya taifa ya Argentina, pamoja na klabu mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles