25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mara yashika mkia matumizi ya vyoo kanda ya ziwa

Shomari Binda -Bunda

MKUU wa Mkoa wa Mara, Adam Malima amesikitishwa na baadhi ya wananchi kutokujenga vyoo kwenye kaya zao na kuwataka watumishi wa idara ya afya kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo.

Akihitimisha kampeni ya uhamasishaji ya ujenzi wa vyoo na usafi wa mazingira, inayoendeshwa na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto jana,  Malima alisema ni aibu la kaya kutokuwa na choo na kujisaidia vichakani.

Alisema kumalizika kwa kampeni hiyo,sasa ni mkakati endelevu kwa watumishi wa idara ya afya kila mmoja kwenye eneo lake kuhakikisha anafanya kazi ya kukagua  vyoo.

Alisema kutokuwa na choo, ni uchafu na hali hiyo haiwezi kukubalika na kumtaka kila mmoja kutimiza wajibu wake wakiwemo wananchi kuhakikisha wanapojenga nyumba wanajenga na choo.

Alisema taarifa za mkoa kuwa wa mwisho kwa mikoa ya kanda ya ziwa kwa matumizi ya vyoo, hazipendezi na kutoa wito wa kila mmoja kubadilika.

“Taarifa hii, sio nzuri kuzisikia masikioni kuwa watu tunaishi bila kuwa na vyoo kwenye kaya zetu ni aibu twende tukahakikishe kila kaya inakuwa na choo kwenye maeneo yetu tunayoishi.

“Kila mahala wapo watumishi wa afya mabwana afya na mabibi afya tembeleeni kaya zote kwenye maeneo yenu na kuhakikisha zinakuwa na vyoo na kuvitumia”,alisema Malima.

Mratibu wa kampeni hiyo kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Anyitike Mwakitalima, alisema Mkoa wa Mara haujafanya vizuri eneo la ujenzi wa vyoo.

Alisema wizara, imekuwa ikitoa motisha mbalimbali kwa mikoa inayofanya vizuri kwenye eneo la afya ikiwemo ujenzi wa vyoo na matumizi sahihi na kuwataka watumishi wa afya kuendelea kuhamasisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles