25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maporomoko ya mawe yatikisa

NA PETER FABIAN, RORYA.

MAPOROMOKO ya mawe na mmomonyoko mkubwa wa ardhi yaliyotokea Kijiji wilayani Rorya  mkoani Mara, yaliyosababishwa na mvua kubwa ya iliyoambatana na upepo mkali, yamesababisha watu 93 kuathiriwa.

Mbunge wa Rorya, Lameck Airo (CCM) alitembelea eneo hilo akiambatana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Charles Ochele na viongozi wengine, walijionea uhalibifu mkubwa wa ardhi uliosabababisha bonde kubwa.

Pia zaidia ekari 20 za mazao, zimesombwa na maji na kuharibiwa.

Akizungumza na wananchi, Airo alisema tukio hilo limeacha maswali mengi na kuwaomba wasamaria wema  kupeleka misaada.

“Tukio hili, limetokea saa 11:00 jioni Desemba 12, mwaka huu, limeacha janga kubwa, mawe na mmomonyoka mkubwa wa ardhi, tushukuru hayakulenga makazi ya wananchi, tungeshuhudia mamia wangepoteza maisha,” alisema.

Airo alisikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Saimon Chacha na kamati yake ya ulinzi na usalama kushindwa eneo la tukio  kujionea hali halisi.

“Nimepokea taarifa za tukio hili kwa mshtuko, nilimtaalifu Ochele na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye, nimekuja na viongozi hawa, tunatoa pole ya Sh milioni 2.3 kwa kaya tatu zilizoathiriwa na kujihifadhi kwa na jirani,”alisema,

Akikabidhi kiasi cha fedha hizo kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Tatwe, Julius Ochwachi,  Airo alisema binafsi ametoa  Sh milioni moja, Ochele alitoa Sh 300,000 na  mdau wa maendeleo aliyefahamika kwa jina moja la Orwero, aliyechangia Sh milioni moja pia.

Mmoja wa wananchi, Kevin Chacha alisema mvua ilianza saa 5:00 asubuhi, ikinyesha kisha ikakata, badae saa 11:00 jioni ikarejea kwa nguvu kubwa.

Ochwachi aliwashukuru kupata msaada huo na viongozi hao kutembelea wananchi kuwafariji.

Alisema waathirika 10, wamepoteza nyumba na mifugo yao, huku wengine 83 wakipoteza mazao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles