30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MAPORI YA AKIBA MATANO KUWA HIFADHI ZA TAIFA

Na MWANDISHI WETU


WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametangaza kuanza kwa mchakato wa kuyapandisha hadhi mapori ya Akiba ya Burigi, Biharamuro, Kimisi, Ibanda, Rumanyika Orugundu kuwa hifadhi za taifa.

Kigwangalla alitangaza uamuzi huo wakati akihitimisha makadirio ya  mapato na matumizi ya wizara yake.

Alisema kupandishwa hadhi kwa mapori hayo yaliyo mkoani Kagera, kutafungua fursa za kukua utalii katika Ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Mapori hayo yapo katika Wilaya za Chato, Biharamuro, Ngara, Karagwe na yanapakana na Hifadhi ya Taifa ya Akagera (Rwanda)

Yanaelezwa kuwa na malisho ya kutosha, mabonde yenye maji mwaka mzima kutokana na kuwepo kwa Ziwa Burigi, Ngoma, Nyarwambaire na Mto Kagera.

Wanyamapori walio kwenye mapori hayo ni pamoja na Simba, Chui, Tembo, Nyati, viboko, Pundamilia, Mamba, Pofu na Pongo.

Inaelezwa pia kuwa, mapori hayo yanapokea wanyama wanaohama kutoka Mapori ya Akiba ya Moyowosi na kufanya Ikolojia ya Magharibi kuwa kivutio cha watalii.

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo jana, ilisema mapori haya yapo katika ukanda muhimu wa kuunganisha watalii kutoka Ikolojia za Magharibi na Mashariki ambapo uwanja wa ndege wa Chato utakuwa muhimu kwa mawasiliano.

“Aidha, barabara kuu kutoka Mwanza, Dar es Salaam kwenda Kigali na Bujumbura, Uganda inalifikia eneo hilo,” inasema taarifa hiyo.

Kwamba kupandishwa hadhi kwa mapori hayo ni mafanikio kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa sababu imeweza kutunza maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi hadi kufikia hadhi ya kuwa hifadhi za taifa.

“Kwa kupandishwa kwake hadhi, uwindaji wa wanyamapori hautaruhusiwa na wanyamapori watatumika kama vivutio vya utalii tu.

“Wizara ya Maliasili na Utalii imelenga kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni nane ifikapo 2025,” inasema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles