23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MAPINDUZI NISHATI MATUMIZI MAKAA YA MAWE

NA FERDNANDA  MBAMILA-DAR ES SALAAM


SERIKALI kupitia Taasisi  isiyo rasmi nchini ya Women in Mining  Netwok  Tanzania (AFWIMNTZ), imetoa msaada wa majiko 238 na kilo 40 za vitofali vya makaa ya mawe katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Taasisi hiyo ambayo makao yake makuu ni Kimara Bucha  jijini Dar es Salaam,  ni taasisi inayotengeneza majiko sanifu  na maalumu kwa matumizi ya  nishati ya vitofali vya makaa ya mawe.

Ofisa Misitu katika Ofisi ya Makamu wa Raisi Idara ya Mazingira, Timothe Mande, anasema kutokana na takwimu za awali nchini, zaidi ya tani laki 3  za misitu hutumika kila mwaka na kuna ongezeko ambalo linategemewa kufikia hadi tani laki 4 mpaka laki 5 kutokana na matumizi ya kuni na mkaa nchini.

Anasema zaidi ya asilimia 30 ya wananchi haswa wa vijijini  hutegemea zaidi matumizi ya kuni na mkaa katika shughuli mbalimbali za kila siku.

Lengo mahususi la mradi huu ni kwamba wajasiriamali hao wanatengeneza majiko maalumu ya makaa ya mawe ili kurahisisha mapishi haswa kwa mama ntilie nchini  kwa kuanza na Manispaa ya Kinondoni.

Kwani baada ya kuanza kutumika kwa majiko hayo, imewarahisisha kwa kiasi kikubwa kwani  hapo awali walikuwa wananunua mkaa wa kawada kwa kiasi cha Sh 6,000  kwa kipimo cha debe, lakini kwa sasa wananunua kiasi cha Sh 3,000 kwa makaa ya mawe.

“Endapo  tutalinda  vyanzo vyetu vya asili kama misitu na vichaka, tutakuwa tumenusuru majanga na maafa mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine yangeweza kutokea hapo baadaye,” anasema Mande.

Anasema ingawa kuna athari za kawaida zinazosababishwa na binadamu na  kutokana na ukataji wa misitu na kwa na uchomaji ovyo  wa vichaka.                 

Hata hivyo, aliipongeza sana Taasisi ya African Women kwa kubuni mradi kama huo ambao umekuwa ni mwanga kwa jamii ya Tanzania kwa ujumla.

Naye Katibu Mtendaji wa Taasisi hiyo, Mary Mbeyela, anasema katika manispaa ya Kinondoni ambapo ina jumla ya kata 20 za wilaya hiyo na 14 za Manispaa ya Ubungo, zimeweza kunufaika na zoezi hilo.

Anasema zaidi ya majiko 170 yenye uwezo wa  kupokea kitofali  kimoja  cha mkaa huo yameweza kutolewa katika ngazi ya Kaya 68 kwa mama lishe na baba lishe, ambayo yana uwezo wa kubeba vitofali  vitatu hadi  vinne kwa wakati mmoja.

“Hata hivyo, majiko yaliyogawiwa tayari kwa baba lishe  na mama lishe, kila jiko moja lina thamani ya Sh 40,000 wakati yale yatakayotolewa kwa ngazi ya  Kaya yana thamani ya Sh 15,000 kwa kila jiko moja,” anasema Mary.

Anasema lengo kuu la  uzinduzi huo  ni kuhamasisha matumizi  ya nishati mbadala ya makaa ya mawe  kwa kuanzia katika nafasi ya kaya hadi manispaa kwa mama lishe  na baba lishe  pamoja na wakaanga chipsi na mishkaki.

Kwani kabla ya kufikia hatua hii ya kutoa msaada wa majiko na makaa ya mawe kwa wananchi hao, taasisi  hii  ilifanya majaribio  ya mkaa huo wa matofali ya mkaa ya mawe ambao ni  wa tofauti zaidi.

“ Kuna baadhi ya taasisi  mbalimbali mfano Gereza la Segerea mnamo  mwaka  2012 lilitoa  msaada pia , Shule ya Sinza maalumu chini  ya mamlaka ya Manispaa ya Kinondoni  mwaka 2013 na  kwenye  majiko ya bwalo  la chakula  katika hostel ya wanafunzi  ya MTC katika Chuo Kikuu cha Sayansi cha Afya Muhimbili,” anasema Mary.

Anasema taasisi imejikita zaidi katika utengenezaji wa  majiko sanifu ambayo ni maalumu kwa  matumizi kwa nishati ya vitofali vya makaa  ya mawe, vinavyotokana na  vumbi  linalopatikana baada ya makaa ya mawe  kusafishwa.

“Utengenezaji wa majiko hayo pamoja na vitofali vya makaa ya mawe , vimefadhiliwa na mfumo wa misitu Tanzania, ambao  uko chini ya   Wizara ya Maliasili na Utalii ili  kusaidia  ukataji ovyo wa misituna, uoto wa asili  hapa nchini,” anasema Mery.

Anasema  baada ya zoezi la uzinduzi huo ambalo limewahusisha watendaji wa  kata na Serikali za mitaa zilizotajwa, watakuwa na jukumu la  kuwatafuta  wananchi  wanaouza  mkaa wa kuni  ili  kuwapa  elimu  juu ya umuhimu wa  kutumia  nishati mbadala na kisha  watawauzia kwa bei  ya jumla  majiko na  vitofali kwa ajili ya kuwauzia wateja wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles