24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mapambano ya kisiasa bado yaitikisa Venezuela

CARACAS, VENEZUELA

WASHAURI wa kiongozi wa upinzani nchini hapa, Juan Guaido wamemtaka kiongozi huyo ateue watendaji wakuu sita wa bodi ya mpito ya kusimamia Shirika la kusafisha petroli la Citgo lililoko nchini Marekani.

Mbali na ushauri huo, kiongozi huyo wa upinzani alitangaza kwamba Februari 23 mwaka huu itakuwa siku ya kuupeleka msaada unaotakiwa haraka nchini kutoka Marekani.

Msaada huo umekwama katika mpaka wa Colombia tangu wiki iliyopita ukisubiri kuingizwa nchini hapa ambako utawala wa Rais Nicolas Maduro unazuia harakati za kiongozi huyo wa upinzani.

Hata hivyo, Guaido hakutoa maelezo kuhusu jinsi msaada huo utakavyoingizwa kutokea mji wa Cucuta nchini Colombia ingawa alisema ataongoza msafara wa magari kuupeleka, hali inayotajwa kwamba inaweza kusababisha hatari inayoweza kuleta vurugu zaidi na mapambano na vikosi vya usalama.

Kiasi cha watu 40 wameshauawa katika mapigano nchini hapa tangu kiongozi huyo wa upinzani mwenye umri wa miaka 35 alipojitangaza kuwa rais wa mpito Januari 23, mwaka huu.

Akizungumza katika mahojiano na Sauti ya Ujerumani (DW), Guaido alisema muda unayoyoma kwa utawala wa Rais Maduro.

“Utawala wa Maduro unaishiwa na muda. Utawala huu hauna mustakabali kwa sababu  Maduro hana mapendekezo na haungwi mkono na wananchi, hana mwelekeo.

“Hawalindi wananchi wake na hilo ni jambo ambalo linakwenda kinyume na vuguvugu linaloungwa mkono na watu wengi na kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

“Pia ni vuguvugu lenye mipango kwa taifa, lina mipango ya kuleta ustawi Venezuela,” alisema kiongozi huyo wa upinzani.

Alisema kwamba jambo hilo haliwezi kuzuilika na inachoweza kufanya Serikali ya Rais Maduro ni kimoja tu ambacho wanakijua zaidi, akitaja kuwa ni kukandamiza, kutesa, kufunga watu au kuzinyakua fedha za Venezuela.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles