MAPACHA WALIOUNGANA WAOMBA WATANZANIA KUWAOMBEA

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Mapacha walioungana, Maria na Consolata Mwakikuti wamewaomba Watanzania waendelee kuwaombea wapone haraka na warejee katika shughuli zao.

Mapacha hao wanaoendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wametoa ombi hilo leo baada ya kuzuka kwa taarifa za kufariki kwao ambapo wameomba taarifa hizo zipuuzwe.

Kwa mujibu wa Ofisa ya Uhusiano wa hospitali hiyo, Neema Mwangomo mapacha hao wanaendelea vizuri na matibabu yao.

Hii ni mara ya pili kwa mapacha hao kuzushiwa kifo, ambapo mapema mwanzoni mwa mwaka huu zilisambaa mtandaoni kuwa wamefariki na Muhimbili walikanusha hizo na kwamba watoto hao hawapo tayari taarifa zao kuandikwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here