25.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Maonyesho ya viwanda vidogo kufanyika Tanga

Susan Uhinga, TangaWafanyabiashara 250 kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, wamejitokeza kushiriki maonyesho ya Biashara ya Kanda ya Kaskazini yalioandaliwa na Shirika la Viwanda Vidogo nchini (SIDO).

Maonyesho hayo yanayotarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Viwanda, George Kakunda, yatafanyika jijini Tanga, katika viwanja vya Tangamano.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela, amesema maonyesho hayo yanayoshirikisha mikoa ya Tanga, Manyara, Arusha na Kilimanjaro yatafanyika kwa siku tano kuanzia Novemba 22, mwaka huu.

“Nawasihi wanachi kujitokeza kwa wingi kwani uwepo wa maonyesho kutatoa fursa ya kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya viwanda na usindikaji.

“Ziko fursa za kujifunza kuelekea ujenzi wa uchumi wa viwanda, tumeona nchi za Afrika Mashariki pia wamejitokeza katika kushiriki,” amesema.

Kwa upande wake Ofisa Uendeshaji wa SIDO, Gladness Foya, amezitaja nchi zilizoonyesha nia ya kushiriki hadi sasa kuwa ni Uganda na Rwanda na kwamba kwa washiriki wenye viwanda vikubwa watashiriki bure huku wasindikaji wakilipia ada  Sh 30,000.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,407FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles