22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Maoni ya viongozi wa Dini kwa JPM

Anna Potinus – Dar es salaam

Rais John Magufuli amezungumza na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu nchi.

Mkutano huo umefanyika leo Januari 23, 2019 Ikulu jijini Dar es salaam ambapo viongozi hao wametoa maoni yao juu ya mambo mbalimbali wanayohitaji yafanyiwe marekebisho.

Mchungaji Amani Lyimo         

Naye Mwenyekiti wa kamati ya wachungaji ya umoja wa Makanisa Mchungaji Amani Lyimo, ataka kuwe na kamati maalum ambayo itaangalia usajili wa madhehebu kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma cha uongozi wa Mwalimu Nyerere ambapo kabla dini mpya haijasajiliwa Wizara ya ndani ilikuwa ikijadili kwanza lakini hivi sasa mambo yamebadilika injili imekuwa kama ni biashara.

Pia ameipongeza Wizara ya elimu ambapo amesemalicha ya kuwa na elimu bure na kama kuna eneo ambalo wazazi wanatakiwa kuchangia waruhusiwe, aidha ameitaka wizara hiyo kuliangalia suala la mikopo ya elimu ya juu kwa jicho la pili hasa kwa watoto masikini wasio na uwezo wa kulipa ada ambao wakati mwingine hushindwa kuendelea na masomo na kurudi nyumbani.

“Ninampongeza Joyce Ndalichako kwa kuimudu Wizara yake lakini kwa elimu ya juu kuna watoto wengi wa masikini wasio na uwezo wamekosa mikopo na kushindwa kuendelea na masomo hivyo ninaomba bodi ya Mikopo iliangalie hili hata sisi viongozi wa dini mkishindwa tutawasaidia, pia kuweze kufanyika uchunguzi maalum maana kuna wenye uwezo wa kulipa lakini bado wanapata mikopo,” amesema Lyimo

Aidha amemtaka rais Magufui kuliangalia suala la demokrasia kwani limewafanya watanzania wengi kuwa na hofu.

“Nikuombe inapowezekana kwa kazi unayoifanya hawatachagua maneno watachagua kazi kama kuna uwezekano waachie pumzi wazungumze ninajua hawawezi kukushinda kwa maneno yao.

Gwajima

Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amepinga kauli ya Mchungaji Lyimo kwa kusema kuwa sio sahihi kusema kusiwe na madhehebu mengi kwani madhehebu yanayohubiri dini ni baraka kwa nchi na kwamba ikiwezekana yaongezeke.

Pia ameitaka serikali kujenga maeneo maalum ya kuabudia katika sehemu za kazi na maeneo mbalimbali ambayo watu watahitaji huduma hiyo ikiwemo viwanja vya ndege.

“Katika viwanja vya ndege wenzetu Waislamu wana maeneo ya kuabudu lakini Wakristo hatuna maeneo hayo kwani hitaji hili ni kwa wote sio kwamba sisi tunaabudu mara moja kwa wiki bali tuna ibada za rohoni kila wakati,” amesema.

Aidha amemuomba rais atoe neno juu ya Askofu Agustine Pemba ambaye amezuiwa kurudi nchini ili aweze kupata kibali cha kurudi.

“Kulitokea mtafaruko kati ya Waislamu na Wakristo kule Mwanza juu ya kuchinja, Askofu mwenzetu Agustine Pemba akaamu kwenda kuishi Marekani lakini amezuiwa kurudi nchini, ikikupendeza utamke neno ili tuweze kuwa naye hapa,” amesema.

Josephat Mwigira

Mtume na nabii wa Kanisa la Efatha Josephat Mwigiraametaka kuwe na mkakati wa utaratibu wa kuweka miundombinu bora kwa kuwa na mipango endelevu kwa miaka ya baadae.

“Utaratibu wa miundombinu ya taifa letu kidogo inaleta kizungumkutu, hatuna mipango endelevu ya miaka 100 kwani watu wanavunjiwa nyumba, vibanda vyao, ni vizuri watu wa barabara, umeme, maji, simu, wakae pamoja wajue namna ya kufanya kazi zao, tuwe na mikakati iliyo bora,” amesema Mwigira

Pia amewataka Wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya kuacha mara moja tabia ya kuwakama viongozi wa dini na kuwaweka ndani kwani kwa kufanya hivyo wanaidhalilisha serikali.

“Viongozi wa Wilaya wanatoa amri za kuweka watu ndani hadi watumishi wa Mungu jambo ambalo sio sawa wengine wanabomoa hadi makanisa ningeomba viongozi wetu wasiwe na mamlaka hayo wanaenda mbali na sasa wanaidhalilisha serikali,” amesema Mwigira.

Amemshauri rais Magufuli kabla hajazipeleka sera zake ni vyema kukawa na utaratibu wa yeye kukutana na viongozi hao wa dini kwanza ili wajadiliane kwa pamoja kwakuwa akifanya peke yake inakuwa ngumu.

Haidar Kamwili 

Mkurugenzi wa hija Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Haidar Kamwili,amesema Kumekuwa na usumbufu kwa vijana wanakuwa wamepata ufadhili wa masomo nje ya nchi wanapofika uwanja wa ndege wanazuiwa kuendelea na safari hata kama wana barua na vibali vinavyowaruhusu kwenda.

“Vijana wetu wanapopata fursa ya masomo nje ya nchi wakifika katika uwanja wa ndege wanawekwa rumande kwa siku hata mbili hata kama wana barua halilali za kuwaonyesha kuwa wana kibali, wakati mwingine wanashindia mikate hivyo ni bora kama kutakuawa na tatizo wakaambiwa maaana wengine wanapelekwa hata sehemu wasizozijua,” amesema.

Aurelian Ngonyani

Askofu Mkuu Kanisa la Truth Minisrty International Aurelian Ngonyani ambaye ameishauri serikali kuwa na utaratibu wa kuwapeleka vijana nchini Israel wakasome kilimo cha kisasa ili wakirudi wasitegemee kilimo cha matone hali itakayopelekea kuifikisha nchi yetu mahali pazuri.

“Eneo kubwa la Israel ni jangwa lakini waisrael wamelifanya kuwa eneo linalozalisha matunda na kulisha mataifa ya Ulaya, je ni kwanini wasipelekwe vijana wakajifunze namna ya kubadilisha jangwa kuwa sehemu ya kilimo, ninaamini huo utakuwa utaratibu mzuri na kuifikisha nchi yetu mahali pazuri,” amesema.

Zainudin Adamjee

Makamu Mwenyeketi Jumuiya ya Mabohora, Zainudin Adamjee ameonesha kukerwa na mchezo wa kamari ambao vijana wengi wamekuwa wakiucheza na kupoteza muda badala ya kujishughulisha na shughuli nyingine za kuwaingizia kipato.

Kikubwa ni kwamba kamari ni haramu lakini hapa nchini vijana wanacheza kamari nje nje kupitia mitandao badala ya kufanya kazi utaona hata kwenye Tv matangazo yanarushwa kila ukiwasha mara utasikia tatu mzuka,” amesema

“Kila siku wanacheza kamari wakifikiria watatajirika halafu wanaposhinda wanapewa zawadi na Mkuu wa Mkoa au wa Wilaya hivyo tatizo kubwa sasa ni nguvu kazi kubwa inacheza kamari zaidi kuliko kufanya kazi,” amesema.

Charles Kitima

Katibu wa baraza la Maaskofu TanzaniaCharles Kitima amepongeza jitihada za serikali na kugusia suala la ajira ambapo amewataka Watendaji wa Wizara mbalimbali kukaa na Wazazi ili kujadiliana namna ya kuunda ajira kwa vijana.

Aidha amesema kuwa wao kama viongozi wa dini wanapinga ndoa isiyokuwa za jinsi moja (isyokuwa ya mwanamume na mwamke) kwasababu hakutakuwa na dunia maana wawili hao hawana uwezo wa kuzaa maana yake dunia itakwisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles