23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maoni: Tushirikiane kudhibiti mauaji haya nchini

Na Salome Bruno

Ndugu Mhariri kwa miezi ya karibuni kumekuwa na mfululizo wa mauaji katika kila kona ya nchi hii.

Vijana kwa wazee, watoto kwa wakubwa kiasi kwamba hatujui kesho kitatokea nini, ni hofu kila mahali.

Kibaya zaidi wale tunaowaamini kuwa walinzi wa familia zetu nyumbani ndiyo kwa namna moja ama nyingine wamekuwa ni chanzo cha mauaji.

Iko wapi sheria na kanuni dhidi ya matukio haya? Ni wazi kwamba Serikali inaendelea kutafakari juu ya suluhu la kudumu la matukio haya ya mauaji ya kikatili yanayotokea mara kwa mara ili yale yanayoweza kudhibitiwa yakomeshe.

Kwani taifa linaendelea kupoteza watoto ambao ndiyo taifa la kesho, wako wapi akina Samia Suluhu Hassan wakesho, tutapata wapi akina, Dk. John Pombe Magufuli wengine kama tutashindwa kudhibiti mauaji haya ya watoto yanayotokea mara kwa mara.

Hivyo, kwa kuhitimisha maoni yangu ndugu Mharirir naomba ndani ya jamii yetu kila mmoja awe ni mlinzi wa mwenzake kwani kila mmoja wetu anayo haki ya kuishi na kulindwa kama ilivyo bainishwa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kila mmoja alinde na kuheshimu haki ya mwenzake.
Mwandishi wa maoni haya ni Mwanafunzi wa Chuo cha Tumaini, Dar es Salaam

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles