28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MAOMBI YA KINA MBOWE YAKWAMA KISUTU

Na KULWA MZEE-DAR ES SALAAM


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeyatupilia mbali maombi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake wanane ya kutaka kesi ipelekwe Mahakama Kuu na kuamuru iendelee kusikilizwa leo mahakamani hapo.

Akitoa uamuzi huo jana, Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri alisema sababu zilizitolewa na upande wa utetezi hazina maana hivyo kesi itaendelea leo   mchana kwa ajili ya washtakiwa hao kusomewa maelezo ya awali.

Waliokuwapo mahakamani wakati uamuzi huo unasomwa ni Mbowe, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Naibu Katibu Mkuu bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika.

Wengine ni Mbunge wa Tarime mjini, Esther Matiko, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk.  Vicenti  Mashinji na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na  Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya hawakuwapo mahakamani, lakini Wakili Peter Kibatala alisema walikuwa safarini kutoka Dodoma   hadi Dar es Salaam kuhudhuria kesi wakaharibikiwa na gari.

Kibatala aliomba kesi hiyo ipangwe kusikilizwa Juni 8 au 15, 2018 kwa sababu  mawakili watakuwa katika kesi Mahakama Kuu.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliomba wawasomee maelezo ya awali leo huku akidai  upande wa utetezi una mawakili zaidi ya wawili na kwamba kutokana na mazingira hayo mawakili waliopo wanaweza kuendelea na kesi leo.

Hakimu Mashauri aliiahirisha kesi hiyo hadi leo saa 8.00 mchana ambako washtakiwa hao watasomewa maelezo ya awali.

Awali, Kibatala aliomba kesi hiyo ihamie Mahakama Kuu kwa hoja kwamba kuna suala la  katiba,  hoja  iliyopingwa na Wakili Nchimbi akidai  hakuna suala la  katiba.

Nchimbi alisema  katika hoja za utetezi hakuna mahali ambako wameshambulia vifungu vya  sheria vilivyotumika kuwashtaki washtakiwa hao, hivyo hoja zao hazina maana.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na   mashtaka 12 katika kesi ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali kinyume cha sheria na kuendelea kufanya mkusanyiko usio halali au maandamano yaliyosababisha kifo cha Akwilina na uchochezi wa uasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles