29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Maofisa watendaji saba kortini

Elizabeth Kilindi- Njombe

TAAISIS ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Njombe, imewafikisha mahakamani maofisa watendaji saba wa vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete kwa tuhuma za wizi wa fedha zaidi ya Sh  milioni 99.

Fedha hizo, ni mali ya halmashauri ya Makete ambazo ni makusanyo ya mapato kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji mapato  POS (Point of Sale electronic Machine).

Akizugumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkuu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Njombe, Domina Mukama alisema wamebaini bado kuna tatizo kubwa eneo la ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali hasa kwa wakusanya mapato waliowekwa na halmashauri maeneo mbalimbali kwa kutumia mashine hizo.

‘’Bado kuna wajanja wachache wanaihujumu Serikali, hasa kwa wausanya mapato kuishia mifukoni mwao,tumefanya uchunguzi na kufanikiwa kuwakamata hawa na kuwafikisha mahakamani,’’alisema.

Aliwatajana watuhumiwa hao, kuwa Chrispin Ngonela (Kijiji cha Matamba), Exavery Mwabena (Kijiji cha Ikungula),Elina Nguvila (Kijiji cha Ndapo),Benson Ambwilo (Kijiji cha Ludodolelo),Salim Salim (Kijiji cha Kisinga),Ebson Mahenge (Kijiji cha Mbalache) wilayani Makete.

Alisema kati ya watuhumiwa hao, wanne ambao mashtaka yao yanazidi Sh milioni 10 wamekosa dhamana kwa kushidwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama.

Watuhumiwa wamekiuka matakwa ya kisheria chini ya kifungu cha 148 (5) (e) cha sheria ya mwenendo wa mashauri ya jinai sura ya 20 marejeo ya mwaka 2002.

Alitoa wito kwa watendaji wa vijiji,kata na watu walioaminiwa na serikali kukusanya mapato ya halmashauri na kuwasilisha kwa usahihi fedha zote katika akaunti za halmashauri.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,609FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles