24.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 29, 2023

Contact us: [email protected]

Maofisa watatu wa polisi wauawa Marekani

Rais Barack Obama
Rais Barack Obama

LOUISIANA, MAREKANI

MAOFISA watatu wa polisi wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa mjini Baton Rouge, Louisiana, ikiwa ni wiki zisizozidi mbili tangu kuuawa kwa polisi wengine watano mjini Dallas.

Mmoja wa majeruhi anaripotiwa kuwa kwenye hali mbaya, huku polisi wakisema mshambuliaji naye aliuawa kwenye eneo la tukio.

Awali polisi walikuwa walifika eneo la tukio, baada ya kupokea simu ikiwaelezea kuwapo mtu mwenye bunduki.

Msemaji wa polisi wa jimbo hilo, Meja Doug Cain, alisema bado hawawezi kuthibitisha ikiwa muuaji alikuwa pekee, na kwa sasa wanawashikilia watu wawili kwa mahojiano.

Hata hiyo, wamemtambua muuaji kuwa askari wa zamani wa jeshi la majini la Marekani mwenye asili ya Kiafrika, Gavin Long, mkazi wa Jiji la Kansas, Missouri.

Long ambaye ameendesha kitendo hicho katika siku yake ya 29 ya kuzaliwa, alilitumikia jeshi la majini kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, akiwa na cheo cha sajini na alikuwa nchini Irak kuanzia mwaka 2008 hadi 2009.

Rais Barack Obama ameyaita mauaji hayo kuwa ni mwendelezo wa machungu kwa taifa ambalo ndiyo kwanza linatafakari matukio ya Dallas.

Akizungumza Ikulu mjini Washington juzi, Obama alisema hakuna linalohalalisha mauaji dhidi ya polisi, na kutaka Wamarekani wajiepushe na maneno na matendo yanayochochea uhasama baina ya raia na vyombo vya dola.

Vyombo vya habari viliripoti Jumapili asubuhi kuwa takriban maofisa saba walikuwa wamepigwa risasi na baadhi yao kukimbizwa hospitalini.

Shambulizi hilo lilitokea saa tatu asubuhi.

Tangu Mmarekani mweusi Alton Sterling kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi katika mji huo mapema Julai, hali ya taharuki imekuwa ikitanda huku mamlaka zikielezea hofu kuwa huenda kukatokea mashambulizi ya kulipiza kisasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles