23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maofisa waonya mambukizi mapya

WASHINGTON, Marekani

MAOFISA wa afya wa ngazi ya juu wa nchini Marekani, wameonya wimbi jipya la maambukizi ya corona.

Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, Robert Redfield alisema kuna hatari ya mlipuko mpya wa ugonjwa wa Covid-19 kugongana na msimu wa mafya.

”athari kubwa sana” kwa mfumo wa afya wa Marekani,” alisema.

Marekani imeshuhudia maambukizi zaidi ya 800,000 ambayo ni ya juu zaidi duniani wakiathirika.

Watu zaidi ya 45,000 wamefariki dunia kufikia sasa kutokana na ugonjwa huo nchini humo kwa mujibu wa takwimu za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

Siku ya Jumatatu,Jimbo la California lilitajwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi mapya, huku mji wa New York, ukiwa na idadi kubwa ya vifo.

Rais Donald Trump, alisema atasitisha maombi ya viza za Green Card ambayo inampa fursa mhamiaji uhalali wa kuwa na kibali cha kuishi Marekani na fursa ya kuomba uraia wa Marekani kwa kipindi cha siku 60.

Chuo kikuu cha Harvard, kimesema kitatoa msaada wa Dola milioni 8.6, licha ya kupata msukumo kutoka kwa Rais Trump kuzirejesha.

Visa vya kwanza vya virusi vya corona katika jimbo la Californiavilionekana mapema zaidi ya walivyofikiria maafisa wa afya walithibitisha. Uchunguzi umebaini kuwa mtu mmoja aliyefariki akiwa nyumbani Februari 6, mwaka huu katika mji wa Santa Clara amejulikana kuwa ni miongoni mwa maambukizi mapya Marekani.Mpaka sasa maambukizi mapya , yanadhaniwa kuwa ni ya mkazi wa Washington ambaye alifariki Februari 26.

Seneta mmoja, alitoa Dola bilioni 484 ili kusaidia ufadhili wa biashara ndogo ndogo, fedha hizo zitasainiwa kutolewa kisheria siku ya Alhamisi.

Katika mahojiano ya kwenye gazeti la Washington Post, Redfield alisema kuwa kuna uwezekano virusi vikarejea upya katika msimu ujao wa baridi, na hali inaweza kuwa mbaya zaidi ya wakati huu.

Aliwataka maofisa wa Marekani kujiandaa kukabiliana na mlipuko mwingine wa mafua makali wakati kama huu.

Alisema upatikanaji wa chanjo unaweza kuwasaidia kuwa na hospitali zenye vitanda ambavyo viko wazi kwa ajili ya wazee ambao watapata virusi vya corona.

Mkuu wa kituo cha kudhibiti magonjwa (CDC) alisema, virusi vya corona vinaweza kuingia Marekani katika msimu wa kawaida wa mafua.

Lakini kama virusi hivyo vinaweza kuibuka wakati ambao kuna msimu wa baridi kali basi hali itakuwa mbaya, mbaya, mbaya sana.

  Tahadhari hiyo imetolewa wakati ambao maseneta wa majimbo mbalimbali nchini Marekani wanaondoa marufuku au wanapunguza masharti ya kutoka nje.

Redfield alisema kuwa watu kuwa kwa mbalimbali ndio jambo sahihi ili kuzuia maambukizi ya virusi hivi vipya, ni muhimu hata makatazo ya mizunguko ifunguliwe.

Maafisa wanapaswa kuchukua hatua ya kuwapima watu ili kufahamu wale ambao wana maambukiz, na watu waliohusiana nao.

Kituo cha kukabiliana na magonjwa kina mpango wa kuajiri watu wengine zaidi ya 650 ili kuweza kuwabaini watu hao.

Anasema, wale waliokuwa wanapinga mafuruku ya kutotoka nje ”haisaidii”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles