24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maofisa lishe watakiwa kupambana na udumavu

MWANDISHI WETU-DODOMA     

MAOFISA Lishe nchini wametakiwa kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuzingatia lishe bora ili kuondoa changamoto ya utapiamlo na udumavu katika jamii.

Akizungumza wakati akifunga mkutano wa siku mbili wa wadau wa lishe uliofanyika jijini Dodoma juzi, kwa niaba ya Waziri wa nchi, Ofisi Waziri mkuu, Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera Uratibu na Uwekezaji,Dorothy Mwaluko alisema kuwa maofisa lishe wanapaswa kuongeza juhudi katika kutoa elimu kwa kushirikiana na wadau kuhusu umuhimu wa lishe bora.

“Kipaumbele lazima kiwekwe katika makundi maalum kama wazee, watoto, akinamama wanajawazito na wale wanaonyonyesha ili kufanikisha azma ya Serikali kuondoa changamoto ya utapiamlo na udumavu hapa nchini,”alisema  Mwaluko

Alisema kuwa Serikali inasisitiza matumizi ya sanaa, vyombo vya habari na viongozi wa kisiasa wakiwemo wabunge katika kuelimisha umma kuhusu athari za utapimlo na udumavu hapa nchini.

Kwa upande wake Katibu mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto (Afya), Dk. Zainab Chaula, alisema kuwa maazimio ya kikao hicho yanapaswa kutoa majawabu yatakayowezesha kuondokana na utapiamlo na udumavu hapa nchini.

Alisema Serikali imeweka mazingira wezeshi ya kufanya kazi na wadau katika kukabiliana na changamoto ya utapiamlo na udumavu katika maeneo yote nchini ili kujenga jamii yenye afya bora.

Dk. Chaula aliwataka washiriki wa mkutano huo kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa sehemu ya mapambano dhidi ya utapiamlo na udumavu hapa nchini ili kujenga jamii yenye afya bora hasa wakati huu Taifa linapojenga uchumi wa viwanda na kutekeleza azma ya kuleta ustawi kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles