25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maofisa habari serikalini kukutana Mbeya

Tunu Nassor -Dar es Salaam

CHAMA cha Maofisa Habari na Mawasiliano Serikalini, (TAGCO),  kimewaomba wakuu wa wizara na idara kuwaruhusu maofisa habari wao kushiriki mkutano wa 15 utakaofanyika Machi 9 hadi 13, jijini Mbeya.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa TAGCO, Paschal Shelutete alisema lengo ni kuwajengea uwezo washiriki kuimarisha idara na vitengo vya mawasiliano na kutangaza shughuli za Serikali.

Alisema kikao hicho kitatathmini kwa kina utendaji kazi wa kipindi cha mwaka mmoja na pia miaka minne ya Serikali ya Rais Dk. John Magufuli.

“Tunawaomba wakuu wa wizara na idara wawaruhusu maofisa habari na mawasiliano kushiriki kikao kazi hicho kwa kuwa kina manufaa katika kuimarisha taasisi wanazozisimamia,” alisema Shelutete.

Alisema kwa sasa zipo changamoto ambazo wanapitia maofisa habari serikalini, ambazo watazijadili kwa kina na kutafuta suluhisho ili kuboresha kazi zao.

 “Tutajadili pia changamoto mbalimbali walizonazo maofisa mawasiliano serikalini, ikiwamo uhaba wa vifaa vya kisasa na kutokushirikishwa katika vikao vya maamuzi na hivyo kukosa taarifa sahihi,” alisema Shelutete.

Alisema lengo lingine ni kukumbushana wajibu wa kuisemea Serikali na kutangaza mafanikio yaliyopatikana kupitia miradi mbalimbali iliyotekelezwa.

“Mwaka huu ni wa uchaguzi, hivyo tutawakumbusha wana mawasiliano hawa kueleza namna ambavyo Serikali imetekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi,” alisema Shelutete. Aliongeza kuwa mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki 500 kutoka wizara, taasisi zinazojitegemea, taasisi na wakala wa Serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles