23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Maofisa Atlabara wauawa Sudan Kusini

 Chabur Goc
Chabur Goc

JUBA, SUDANI KUSINI

Maofisa wawili wa mabingwa wa soka nchini Sudan Kusini, klabu ya Atlabara, wameuawa na watu wasiojulikana kutokana na machafuko yaliyotikisa mji mkuu wa Juba wiki iliyopita.

Shirikisho la Soka la Sudan Kusini (SFA), limetangaza kuwa maofisa hao walivamiwa na kupigwa risasi na watu wasiojulikana, usiku wa kuamkia Jumamosi.

Rais wa SFA, Chabur Goc, aliwataja viongozi hao kuwa ni William Batista na Leko Nelson.

“Shirikisho la soka nchini Sudan Kusini, linasikitika kutangaza vifo vya viongozi wa mabingwa watetezi wa klabu ya Atlabara, ambao wamepigwa risasi na watu wasiojulikana, ni jambo la kusikitisha, pia ni pigo kubwa kwa soka la Sudan.

“Uchunguzi unaendelea kufanyika kuwatafuta wahusika wa tukio hilo, na tunaomba Mwenyezi Mungu awaweke mahali pema peponi,” alisema Goc.

Kwa upande wao, uongozi wa Atlabara umesema kuwa umeguswa na vifo vya viongozi hao na kwamba wapo pamoja na familia za marehemu katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Batista alikuwa katibu mkuu katika klabu hiyo wakati huo Nelson alikuwa akihudumu kama meneja mkuu wa Atlabara.

Mapigano nchini humo yamekuwa yakiendelea kwa siku za hivi karibuni kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kiir na wanajeshi watiifu kwa makamu wa kwanza wa Rais Dk. Riek Machar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles