27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MANYARA KINARA KWA MATUKIO YA UKEKETAJI

NA CHRISTINA GAULUHANGA,
DAR ES SALAAM

SERIKALI imeandaa mpango mkakati wa miaka mitano kuhakikisha vitendo vya ukeketaji vinatokomezwa, huku ikitaja Mkoa wa Manyara kuwa kinara wa matukio hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuzuia Ukeketaji inayofanyika leo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Magreth Musai, alisema mpango huo wa mwaka 2017/2022 utasaidia kupunguza matukio hayo kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.

Alisema mpango kazi huo umeainisha maeneo nane muhimu, mojawapo ikiwa ni kuondoa mila na desturi zenye madhara.

“Mikoa inayoongoza kwa ukeketaji  na asilimia zake kwenye mabano kuwa ni Manyara (58), Dodoma (47) na Arusha (41),” alisema.

Magreth aliongeza kuwa takwimu za Tafiti ya Idadi ya Watu na Afya (TDHS 2010), zinakadiria ukeketaji kwa wasichana na wanawake wenye umri wa miaka 15-49 kuwa ni asilimia 14.6, hali inayoonyesha kupungua ukilinganisha na asilimia 17.9 ya mwaka 1996.

Pia alisema takwimu hizo kwa mwaka 2015/2016 zinaonyesha kiwango cha ukeketaji kwa wanawake na watoto kimepungua kutoka asilimia 14.6 ya mwaka 2010 hadi kufikia asilimia 10.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Jinsia kutoka wizara hiyo, Julius Mbilinyi, alisema Serikali imetunga sera, sheria, miongozo na kuandaa mikakati mbalimbali katika jitihada za kupambana na tatizo hilo.

 “Malengo yetu ni kupunguza vitendo vya ukatili kutoka asilimia 39 mpaka asilimia 20 na kutoa mafunzo mbalimbali  ambapo hadi kufikia mwaka 2016, jumla ya wasichana 2,331 walipatiwa mafunzo  huku wanafunzi wa kike 46 walikimbia ukeketaji,” alisema Mbilinyi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles