27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Manukato, sabuni huathiri afya ya uke

VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

WANAWAKE wanaotumia manukato kujifukiza ukeni na wale wanaotumia sabuni mbalimbali kujisafisha, wametahadharishwa kwamba wanajiweka kwenye hatari ya kupata magonjwa mbalimbali ikiwamo saratani.

Hayo yalielezwa juzi jijini hapa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Hellen Makwani alipozungumza kwenye mahojiano maalum.

Daktari huyo alisema hata kemikali zinazotumika kwa madai ya kurejesha bikra nazo zinaweka afya ya uke hatarini.

“Kimaumbile, uke hujisafisha wenyewe, una jinsi ambavyo hutoa majimaji ambayo huusafisha na kutoa uchafu ambao upo ukeni, mwanamke anaweza kujisafisha bila hata kuingiza kidole na uke wake ukawa salama.

“Hatupendi watu waone kutumia manukato na sabuni ni salama kwao, kwa sababu ukeni kuna bakteria maalum ambao huufanya ujisafishe wenyewe, zile kemikali huenda kuua wale bakteria, matokeo yake uke unaanza kupata maambukizo ya mara kwa mara.

“Kujisafisha kwa sabuni kunaweza kusababisha michubuko kwenye uke kwa sababu wenyewe una ngozi nyembamba, hali hiyo humuweka mwanamke kwenye hatari ya kupata maambukizo kwa urahisi kwa mfano HIV pindi anapojamiana.

“Aidha, tunaona pia saratani nyingi zinahusiana na HIV hasa kirusi cha HPV (Human Papilloma Virus) ambacho husababisha saratani ya kizazi, ni rahisi kupata upenyo na kufanya mabadiliko katika seli za mwili,” alibainisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles