24.3 C
Dar es Salaam
Monday, September 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mansour atoa Milioni 5 ujenzi wa ofisi ya CCM Tangini, ahimiza ushirikiano

Na Gustafu Haule, Pwani

MJUMBE wa kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani Musa Mansour, ametoa, Sh milioni tano na matofali 2,000 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Tangini iliyopo katika Jimbo la Kibaha Mjini.

Mansour ametoa mchango huo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa ofisi hiyo iliyofanyika juzi iliyoendeshwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Silvestre Koka .

Akikabidhi fedha hizo kwa mbunge, Koka mbele ya viongozi mbalimbali wa CCM Kata ya Tangini, Wilaya na Mkoa, Mansour amesema kujenga chama kunahitaji ushirikiano.

Aidha, Mansour amesema kuwa pamoja na kutoa mchango huo lakini bado ataendelea kushirikiana na viongozi wa pamoja na wanachama wa CCM kuhakikisha ofisi hiyo inakamilika kwa wakati.

Amesema kujenga chama ni jukumu la wanachama wote hivyo kinachotakiwa ni kushirikiana kwa kila Jambo ili kuhakikisha wanazidi kukiimarisha chama hasa katika ushindi wa chaguzi zijazo.

“Leo natoa mchango huu wa milioni tano na matofali 2000 kwa ajili ya kujenga ofisi yetu ya CCM Kata ya Tangini lakini nitakuwa nanyi muda wote kuhakikisha ofisi inakamilika kwa wakati,” amesema Mansour.

Aidha, Mansour amewaomba viongozi na wanachama hao kuhakikisha wanaanza kujipanga katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika 2024 kwakuwa kushinda kwa uchaguzi huo ni dira ya ushindi wa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Tangini, Anthony Milao, amemshukuru Mansour kwa mchango huo mkubwa huku akisema watakwenda kuutumia kikamilifu katika kutekeleza mpango wa ujenzi wa ofisi hiyo.

Hata hivyo, katika harambee hiyo mbunge Koka alifanikiwa kukusanya zaidi ya Sh milioni 15 .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles