22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

MANJI AUGUA JELA

PATRICIA KIMELEMETA NA MANENO SELANYIKA

MFANYABIASHARA Yusuf Manji jana alishindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa ajili ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mgonjwa.

Wakili wa Serikali, Estazia Wilson, alieleza hayo mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa.

Wakili Estazia alidai kuwa, jambo hilo limemfanya Manji ashindwe kufika mahakamani kusikiliza kesi yake wakati shauri lilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa.

 

Wakili huyo alidai kuwa, taarifa za kuugua kwa Manji alizipata kutoka kwa Askari Magereza, kabla ya kuingia mahakamani na kwamba alipewa (ED) ya siku mbili ili aweze kupumzika.

Pamoja na hilo, washtakiwa wenzake na mfanyabiashara huyo, Deogratias Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwere, walifika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi yao.

 

Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 25, mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa.

 

Katika kesi hiyo, Manji na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba chini ya sheria ya uhujumu uchumi na usalama wa Taifa kwa kukutwa na vitambaa vya kutengenezea sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 na mihuri.

Manji na wenzake wanadaiwa kuwa, Juni 30, 2017, katika eneo la Chang’ombe ‘A’ Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, walikutwa na askari polisi wakiwa na bunda 35 za vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za Jeshi la Wananchi Tanzania, zenye thamani ya Sh milioni 192.5 na kwamba mali hiyo ilipatikana kinyume cha sheria.

 

Katika shtaka la pili, wanadaiwa Julai Mosi, 2017, huko Chang’ombe ‘A’, washtakiwa hao walikutwa na polisi wakiwa na mabunda nane ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za JWTZ, zenye thamani ya Sh milioni 44, mali ambayo ilipatikana isivyo halali.

 

Katika shtaka la tatu, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuwa Juni 30, 2017 Chang’ombe ‘A’, walikutwa na muhuri wa JWTZ wenye maandishi, Mkuu 121 kikosi cha JWTZ bila ya kuwa na uhalali, kitendo ambacho kingehatarisha usalama wa nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles