30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

Manji augua, apelekwa Muhimbili

                                                       

MFANYABISHARA  maarufu  nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, ameonekana  Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam akichukuliwa na gari la wagonjwa aina ya Land Cruiser na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Manji ni miongoni mwa watu 65 waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika sakata la dawa za kulevya wiki iliyopita.

Timu ya waandishi wa MTANZANIA ambayo jana ilikuwa imepiga kambi katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, ilishuhudia mfanyabishara huyo akitembea na kupanda katika gari la gari la Wagonjwa aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili za DFP na kuondoka naye huku gari lake aina ya Range Rover  namba ya usajili T 538 DHY likitangulia mbele.

Wakati Manji anachukuliwa na gari hilo la wagonjwa hakuwa amebebwa ila alikua akitembea mwenyewe na kuingia kwenye gari hilo ambalo lilielekea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ingawa haijafahamika anaumwa nini mfanyabishara huyo.

MTANZANIA ilipomtafuta kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro, alisema suala la linalohusu watu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za dawa za kulevya atalizungumzia leo.

“Kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote hadi kesho (leo),” alisema Sirro na kukata simu

Alipotafutwa Meneja Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Eligaesha ili kupata ufafanuzi wa kupokewa kwa Manji hospitalini hapo simu yake haikupatikana hadi tunakwenda mitamboni.

Wakati hayo yakiendelea Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Idd Azzan, jana aliachiwa na kutoka polisi ambapo alikuwa akishikiliwa kwa siku mbili mfululizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles