29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Manispaa Mpanda yapunguza hoja za CAG

Walter Mguluchuma -Katavi

HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, imefanikiwa kujibu hoja 76 kati ya 125 zilizotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), katika mwaka wa fedha 2017/18 zikiwa zimejumuisha hesabu za miaka ya nyuma jambo lililochangia kuipa hati safi.

Hayo yalisemwa jana na Mkaguzi Mkuu wa Nje, Mohamed Msangi katika kikao cha Baraza la Madiwani ambacho kilikuwa kinajadili hoja za taasisi hiyo ya ukaguzi.

Alisema utekelezaji wa maoni ya taasisi hiyo kwa Manispaa ya Mpanda ni wa kuridhisha, kwani kati ya hoja 125 zilizotolewa mwaka wa fedha 2017/18  zikijumuisha na  hoja  za miaka ya nyuma, 76 zimepatiwa majibu ya kuridhisha na kufungwa huku 49 ambazo ni sawa na asilimia 39 zimebaki.

Msangi alisema hoja zilizosalia zimegawanyika makundi mawili ambapo la kwanza ni zilizopatiwa majibu yasiyoridhisha huku nyingine zikipatiwa majibu lakini bado zinaendelea kutekelezwa kwa hatua ya ufuatiliaji.

Alieleza kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda  ilifanyiwa ukaguzi wa hesabu na CAG kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2018 na ripoti ya ukaguzi kukabidhiwa Rais Machi 28, mwaka huu na kuwasilishwa bungeni Aprili 10.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda, Michael Nzyungu, alisema manispaa hiyo itahakikisha hoja zilizobaki   zinamalizwa kadiri ambavyo wameelekezwa kufanya na CAG.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera, aliiagiza   manispaa hiyo kuhakikisha mikataba yote ya miradi ya maendeleo inasainiwa kwa wakati na fedha zinatumika vizuri ili waweze kuepukana na hoja za CAG.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles