20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

MANISPAA LINDI YAKUSUDIA KUMALIZA TATIZO LA UCHAFU

                                                                      Hadija Omary, LindiWakazi wa Wilaya ya Lindi, mkoani Lindi wamekusudia kumaliza tatizo la uchafu wilayani humo kwa kununua matela matano yenye thamani ya Sh milioni 60, yatakayotumika kama maeneo ya kukusanyia taka kwa sehemu zisizo na vizimba katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani humo.

Akizungumza wakati hafla fupi ya uzinduzi wa matela hayo wilayani hapa, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shahibu Ndemanga pamoja na mambo mengine ameupongeza uongozi wa halmashauri hiyo ya kwa kuwa na mipango mizuri ya kuhakikisha manispaa inakuwa na vitendea kazi vya kisasa  vya kufanyia usafi.

“Huwezi kukusanya taka wakati huwezi kuzizoa na kupeleka dampo huwezi kuwa na vifaa vya kuzolea taka wakati huna dampo, unakwenda kutupa wapi takataka?

“Mmeamua kujenga dampo, mmenunua lori kwa ajili ya kubeba takataka mmenunua Kijiko kwa ajili ya kupakilia taka taka na leo mmenunua vizimba ambavyo vinatembea ni uamuzi mzuri na Manispaa tuendele kufanya hivyo,” amesema  Ndemanga.

Aidha, Ndemanga pia ametoa wito kwa wananchi kuyatunza matela hayo dhidi ya uharibifu na hujuma mbali mbali zinazoweza kuzuilika kwani yatawekwa kwenye maeneo wanayoishi, ili yaweze kudumu kwa kutumika kwa muda mrefu.

Awali akisoma taarifa ya ununuzi wa matela hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi,  Jomary Satura Afisa mazingira wa Halmashauri hiyo Vavenalis Mauna amesema matela hayo yana uwezo wa kubeba taka kati ya tani sita hadi saba kila moja na yana uwezo wa kumwaga taka yenyewe kwa kubinuka.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles